Nafasi Ya Matangazo

March 08, 2022

Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wananchi wa Jimbo la hilo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kijiji Cha Msolwa Kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani.
Wananchi Hao walimweleza Mbunge wao kuwa, Serikali ilitoa Sh millioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.

"Mara baada ya kukamilika Kwa ujenzi  wa shule hii, tunaamini kiwango Cha ufaulu kitaongezeka na kusaidia kupatikana Kwa watalaam wa fani mbalimbali ambao wataitumikia nchi Yao,tunawaomba wazazi na walezi kushirikiana na serikali Kwa ajili ya kuwashawishi wanafunzi kupenda kusoma," alisema Ridhiwani.
Posted by MROKI On Tuesday, March 08, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo