Waziri wa Maji Mhe. Jumaa
Aweso (Mb) amewataka watendaji wa sekta ya maji kuzingatia weledi na miongozo
ya Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maji.
Amesema kwa sasa kazi inaendelea na inaridhisha kwa mwenendo wake ila watendaji wasijisahau na kuharibu yaliyo mema.
Waziri Aweso amesema hayo leo Februari 23, 2023 aliooongea katika uzinduzi wa matokeo ya tathmini ya utendaji programu ya Lipa kwa matokeo ( Pay by Result) awamu ya 6 (PbR6) naLipa kutokakana na Matokeo, (Pay for Result awamu ya Pili (PforR2).
Aidha, Aweso ametumia dakika 30 kuendesha kikao na Menejimenti ya Wizara ya Maji, na taasisi zake ikiwamo, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mabonde ya Maji, Mamlaka za Maji na Chuo cha Maji.
Aidha, amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ana matumaini makubwa ya kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa Watanzania kupitia rasilimali watu aliyo nayo ndani ya Wizara ya Maji.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesisitiza ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za sekta ya Maji.
“ Tuendelee kusadiana kutimiza majukumu yetu. Tufahamu kwamba sisi sote ni Wizara ya Maji bila kujali kwamba huyu ni RUWASA, huyu ni Mamlaka ya Maji au Bonde la Maji. Hakikisha kila wakati unachukua hatua mambo yote yaende vizuri” Amesema Mhandisi Mahundi
Katika tukio hilo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesisitiza umuhimu wa kutunza takwimu ili kuweza kufanya maamuzi yaliyosahihi katika kutoa huduma kwa Umma.
“Watumishi wa sekta ya maji mhakikisha mnakusanya, mnachakata mnahifadhi na kutoa takwimu sahihi kwa ajili ya mipango ya wizara. Eneo la Takwimu ni eneo muhim ambalo linaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupanga mipango ya Wizara.”
Kufuatia matokeo ya tathmini, Waziri Aweso ametoa zawadi kwa Watendaji mbalimbali wa RUWASA katika ngazi ya mikoa na wilaya zilizofanya vizuri katika program tofauti tofauti ambapo mkoa wa Tabora umeongoza kwa upande wa program ya PforR2 wakati Njombe ikiongoza kwa program ya PbR6




0 comments:
Post a Comment