Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akikagua kituo cha maunganisho ya Mkongo wa
Mawasiliano wa Taifa wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya
mkongo huo kutoka Manyoni, Singida
mpaka Kambikatoto mkoani Mbeya.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari Mhandisi Nikusubila Maiko akifafanua jambo kwa
Katibu Mkuu Wizara hiyo,
Dkt. Jim Yonaz juu ya ubora
wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu
huyo ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya mkongo huo
kutoka Mnyon, Singidai mpaka Kambikatoto, Mbeya

Mkurugenzi
wa TEHAMA kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa
Munaku akielezea jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi wakati Katibu
Mkuu huyo
alipofanya ziara kukagua ujenzi wa miundombinu ya mkongo huo kutoka Manyoni, Singida mpaka Kambikatoto mkoani
Mbeya.
Mhandisi
wa kuunganisha waya wa Mkongo,
Evanda Luvanda wa Kampuni ya Raddy Fibre Solution,
akieleza urefu na ubora wa mkongo huo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi wakati wa ziara ya Katibu Mkuu
huyo kukagua ujenzi wa
miundombinu ya mkongo huo kutoka Mnyoni, Singida
mpaka kambikatoto, Mbeya.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akisoma kipimo kinachoonesha
urefu na ubora wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa akiwa kwenye kituo cha kutolea huduma za Mkongo cha Rungwa
wakati ziara yake ya kukagua
ujenzi wa miundombinu ya mkongo huo kutoka Manyoni, Singida mpaka Kambikatoto mkoani Mbeya.
***********
Prisca Ulomi na Daudi Manongi, Kambikatoto
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Dkt. Jim Yonazi amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA yenye
urefu wa kilomita 265 ambao umefanyika kwenye eneo la Itigi, Manyoni mkoani
Singida hadi eneo la Kambikatoto, Mbeya. Ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu hiyo
ni pamoja na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wenye urefu wa kilomita
265, vituo vya kutolea huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na vituo vya
kuongeza nguvu za mawasiliano.
Dkt. Yonazi amesema kuwa amefanya ziara hiyo ili kukagua ujenzi huo kwa
lengo la kujiridhisha na maendeleo ya ujenzi huo ili kuona namna mkandarasi
ametekeleza kazi husika kwa kuwa Serikali imetoa shilingi bilioni nane za
kufanikisha ujenzi wa miundombinu hiyo iliyojengwa eneo la Itigi, Manyoni hadi
Kambikatoto
Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata
huduma bora za mawasiliano, za uhakika na kwa gharama nafuu katika maeneo yote
nchini nzima ili kuhakikisha kuwa mawasiliano yanaendelea kutumika katika shughuli
za kiuchumi na kijamii katika kuchochea maendeleo ya taifa letu
Naye Meneja Mradi wa ujenzi wa miundombinu hiyo, Rajab Mikumwo wa Kampuni
ya Raddy Fibre Solutions ambaye ni mkandarasi
aliyejenga miundombinu hiyo amemweleza Dkt. Yonazi kuwa, kampuni yao imetekeleza
ujenzi wa miundombinu hiyo kwa mujibu wa matakwa ya mkataba na tayari nyaya za
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano zimelazwa ardhini na katika baadhi ya maeneo nyaya
hizo zimepitishwa juu ya nguzo kuendana na jiografia ya eneo husika endapo kuna
mto au mwamba ili kuhakikisha kuwa mawasiliano yanapatikana kwa uhakika mwanzo
hadi mwisho wa eneo husika
Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Mulembwa Munaku amesema kuwa tayari
Serikali imefikisha miundombinu hiyo kwenye maeneo ya mipaka ya nchi za jirani
zinazopakana na Tanzania na sasa hatua zinaendelea za kufikisha mawasiliano
hayo mpakani mwa DRC Congo na Tanzania ili nchi jirani ziendelee kutumia na
kunufaika na miundombinu hiyo
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wizara hiyo,
Mhandisi Nikusubila Maiko emesema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo utawezesha watoa huduma za mawasiliano
nchini kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi kwa kuwa tayari watoa
huduma hao wamewasilisha mahitaji hayo Wizarani ambapo ujenzi wa miundombinu hiyo
utaongeza kasi ya matumizi ya TEHAMA kwa taasisi za Serikali, sekta binafsi na
wananchi walio kwenye maeneo hayo ambapo miundombinu hiyo imejengwa.
0 comments:
Post a Comment