Baadhi ya mitambo ya kuchakata Gesi ya
Madimba mkoani Mtwara.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali wakiwa katika mitambo ya kuchakata Gesi ya Mnazi
Bay mkoani Mtwara. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali wakiwa katika kituo cha kupokea Gesi cha Kinyerezi
jijini Dar es Salaam ambacho husambaza Gesi katika maeneo mbalimbali ikiwemo
kwenye mitambo inayozalisha umeme ya Kinyerezi I na II.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali wakiwa katika chumba cha kuendeshea mitambo katika
kituo cha kupokea Gesi cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam ambacho husambaza
Gesi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mitambo inayozalisha umeme ya
Kinyerezi I na II. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James
Mataragio.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali wakiwa katika chumba cha kuongozea mitambo cha Madimba
mkoani Mtwara.Aliyekaa ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Naghenjwa Kaboyoka.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali wakiwa katika mitambo ya kuchakata Gesi ya Madimba
mkoani Mtwara. Wengine ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati na TPDC.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakiwa katika
picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mitambo ya kuchakata Gesi Asilia ya
Mnazi Bay mkoani Mtwara. Wa Pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mhe.Naghenjwa Kaboyoka.
*************
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali, imetoa wito kwa Serikali kuwa, suala la usambazaji gesi majumbani
liwe ni la kipaumbele.
Wito huo umetolewa kupitia kwa Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Mhe.Naghenjwa Kaboyoka jijini Dar es Salaam mara baada ya ziara ya
Kamati hiyo kutembelea miundombinu mbalimbali ya Gesi iliyopo mkoani Mtwara,
Pwani na Dar es Salaam.
Alisema kuwa usambazaji wa Gesi hiyo
majumbani uzingatie kupeleka nishati hiyo kwenye maeneo yenye watu wengi ili
kuweza kupunguza matumizi makubwa ya mkaa ambayo yanapelekea ukataji wa miti na
hivyo kuleta uharibifu wa mazingira.
Kuhusu ziara ya Kamati hiyo kwenye
miundombinu ya Gesi alisema kuwa, Kamati imeona uwekezaji mkubwa uliofanyika na
kufurahishwa na jinsi wafanyakazi watanzania wanavyoendesha na kusimamia
miundombinu hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,
Dkt. James Mataragio aliieleza Kamati hiyo kuwa, kazi ya usambazaji Gesi
majumbani inaendelea katika mikoa mbalimbali na kwamba ili gesi hiyo isambazwe
kwa wananchi wengi zaidi, wameanza kukaribisha kampuni binafsi ili ziweze
kusambaza nishati hiyo majumbani.
Ziara ya PAC ilikuwa na malengo mbalimbali
ikiwemo kuona kama ujenzi wa miundombinu ya Gesi iliyopo inalingana na thamani
ya fedha iliyotolewa.
Wajumbe wa PAC walitembelea mitambo ya
kuchakata gesi ya Mnazi Bay ambapo Gesi hiyo husafirishwa kwenda Mtwara Mjini
ili kuzalisha umeme unaotumika katika mikoa ya Mtwara na Lindi na Gesi nyingine
hupelekwa kwenye mitambo ya kuchakata Gesi ya Madimba inayomilikiwa na TPDC.
Aidha, Kamati hiyo pia ilitembelea visima vya
gesi vitano vilivyopo nchi kavu katika eneo hilo la Mnazi Bay mkoani Mtwara, nyumba
zilizounganishwa na Gesi Asilia kwa ajili ya kupikia na matoleo ya Bomba kubwa
la Gesi ambayo hupeleka Gesi maeneo
mbalimbali ikiwemo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo mkoani
Mtwara.
Aidha, wajumbe hao wa Kamati walitembelea
mitambo ya kuchakata Gesi Asilia iliyopo Madimba yenye uwezo wa futi za ujazo
milioni 210 ambapo gesi hiyo baada ya kuchakatwa husafirishwa kwa Bomba kubwa
linalotoka eneo hilo mpaka mkoani Dar es Salaam na hivyo kuwezesha gesi hiyo
kutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, kutumika viwandani
kwenye magari na majumbani.
Vilevile Wajumbe hao walitembelea vituo vya
kupokea Gesi iliyochakatwa vya Somanga mkoani Lindi na Kinyerezi jijini Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment