Nafasi Ya Matangazo

July 28, 2021

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Mhandisi Zana Ahmed Said akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Prof. Charles Mgone akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 16 ya Sayansi, Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wakuu wa Taasisi za  Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia waliohidhuria maonesho ya 16 ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungunzi wa maonesho hayo yanayofanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari Zanaki wakijibu maswali wakati walipotembelea maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Mhandisi Zana Ahmed Said akwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kifungua  maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.
********"

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said amesema Taasisi za Elimu ya juu zina wajibu wa kufanya tafiti zinazojikita katika kutatua changamoto za jamii na kuiwezesha kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika pato la Taifa.​
Balozi Zena amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yenye kauli mbiu “Kuendelea Kukuza na Kudumisha Uchumi wa Kati kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia”. ​
Amezitaka Taasisi hizo kujitathmini ni kwa namna gani zimekuwa sehemu ya ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii na kuwa chachu ya maendeleo ya taifa na kushirikiana kwa karibu na Sekta Binafsi naTaasisi za Utafiti na Maendeleo ​ ili kuweka utaratibu wa kuendeleza teknolojia zinazozalishwa nchini na kuhamasisha matumizi yake kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. ​
“Kupitia Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu tunapata rasilimali watu yenye maarifa na ujuzi unaohitajika kwenye sekta zote, na pia tunapata matokeo ya tafiti na bunifu zinazolenga kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii,” amesema balozi Zena.​


Aliongeza kuwa Sekta ndogo ya Elimu ya Juu ni mhimili mkubwa na chachu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Katika Karne hii ya 21, taasisi za Elimu ya Juu zina jukumu kubwa zaidi la kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaaluma na kitaalamu kuhusu dira na mwelekeo wa jamii yetu na taifa kwa ujumla. 

“Tafiti zinaonesha kwamba, ili kuweza kudumu na kukua ndani ya uchumi wa kati wa juu, inabidi nchi iwe na rasilimaliwatu ya ujuzi wa juu ya asilimia 12 na Ujuzi wa kati asilimia 26. Kwa takwimu za mwaka 2016 wenye ujuzi wa hali ya juu ni asilimia 3.3 wakati wale wa ujuzi wa kati ni asilimia 17. Hii inaonesha kwamba bado Taasisi zetu za Elimu ya Juu zina kazi kubwa ya kuongeza wataalam wa kiwango cha ujuzi wa juu na wa kati”,alisema balozi Zena. 

Aidha alisema  ushiriki wa wanafunzi wetu katika Elimu ya Juu kwa sasa ni asilimia 6.1 ambapo bado tupo nyuma ya wastani wa nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ambao ni asilimia 9.4  na pia tupo nyuma ya jirani zetu wa Kenya ambao kwa takwimu za 2018 walikuwa na ushiriki wa asilimia 11.

“Wastani huu bado upo chini sana, hivyo ni muhimu kuendelea kuweka mipango itakayoongeza idadi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu wenye ujuzi na maarifa yanayotakiwa sokoni,”aliongeza Balozi Zena.

Aidha Balozi Zena ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, kuongeza jitihada katika uthibiti wa ubora wa vyuo vikuu nchini ili kuhakikisha vinafuata taratibu zilizopo ili kutoa elimu iliyokusudiwa. Aidha pamoja na kusimamia taaluma, amevitaka kujikita pia kwenye kusimamia masuala ya utafiti na ushauri katika Vyuo Vikuu. 
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Prof. Charles Mgone amesema wataendelea kuimarisha mifumo ya uthibiti ubora wa elimu ya juu na kufanya​Taasisi hizo kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa na kuzalisha wahitimu mahiri, wabunifu​ wenye uwezo wa kusaidia ushindani wa soko la ajira na changamoto za kijamii na kiuchumi.​

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amesema kufanyika kwa maonesho hayo ni fursa kwa wanaotaka kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kupata taarifa nyingi za vyuo kwa wakati mmoja na kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule mbalimbali waliohudhuria maonesho hayo kupata taarifa ya kozi zitakazowafaa baada ya kuhitimu na kwamba udahili unafanyika moja kwa moja kutokea katika viwanja vya maonesho.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Prof. Charles Kihampa amesema lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa Taasisi zinazoshiriki kujitangaza kwa kuonesha huduma, kazi mbalimbali wanazofanya na mchango wao katika kuendeleza jitihada za Serikali za kukuza na kudumisha uchumi wa Kati kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknnolojia.​
Amesema katika maonesho ya 2021 jumla ya Taasisi 73 zimeshiriki ambapo ni Taasisi zinazotoa mafunzo kwa ngazi ya elimu ya juu, mabaraza ya Uthibiti ubora, wakala na Taasisi nyingine za Serikal, Bodi za usajili wa wataalamu, Taasisi za Sayansi Teknolojia na utafiti na Taasisi za Huduma za kifedha​na Wakala wa Vyuo Vikuu vya Nje.​
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliofika katika maonesho hayo wameishukuru Tume ya Vyuo Vikuu nchini kwa kuwa na maonesho hayo kwa kuwa yanakutanisha Vyuo Vikuu vyote sehemu moja na kurahisha upatikanaji wa taarifa za kujiunga na vyuo hivyo bila kutumia gharama ya kusafiri kutafuta vyuo vilipo.​
Posted by MROKI On Wednesday, July 28, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo