Nafasi Ya Matangazo

January 25, 2019

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo ameendelea na ziara yake mkoani Geita ambapo ametembelea mradi wa ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA kinachojengwa Wilayani Chato mkoani humo na kusema kuwa ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo ameendelea na ziara yake mkoani Geita ambapo ametembelea mradi wa ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA kinachojengwa Wilayani Chato mkoani humo na kusema kuwa ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Chuo hicho Waziri amesema upo upungufu wa vyuo vya kutolea mafunzo ya Ufundi na tayari serikali imeendelea kujenga ili kuhakikisha dhamira ya kuwa nchi ya viwanda inafikiwa.

Waziri Ndalichako ameendelea kuitaka Idara ya manunuzi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha inafanya uchaguzi sahihi wa mkandarasi na kuwa hilo ndiyo suluhisho la kukamilisha miradi ya ujenzi kwa wakati.

“Nitumie fursa hii kuzielekeza halmashauri zote nchini kuendelea kukamilisha majengo na majengo yakishakamilika basi Wizara tutanunua vifaa kupitia mradi wa kukuza ujuzi na kazi (ESPJ) lengo la serikali ni kuendeleza ujuzi ili kupata wataalamu wa kutosha,” alisema Prof. Ndalichako.

Akiwa Wilayani Chato, Waziri Ndalichako alizungumza na wanafunzi wa kidato Cha tano na sita wa shule ya sekondari ya wasichana ya Jikomboe ambapo ameahidi kutoa kiasi Cha Tsh. Milioni mia mbili kwa ajili ya kujenga bwalo, chumba cha darasa na kumalizia uzio wa shule hiyo.

Waziri Ndalichako kesho ataendelea na ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi ya vyuo vya Ufundi stadi mkoani Kagera.
Posted by MROKI On Friday, January 25, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo