Nafasi Ya Matangazo

January 25, 2019

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (katikati) akikagua ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Geita.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru kuchunguza mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya ujenzi wa mradi wa Chuo Cha Ufundi stadi VETA mkoani Geita unaotekelezwa na kampuni ya ukandarasi inayojulikama kama SkyWard.

Waziri huyo amesema hajaridhishwa na ujenzi wa mradi huo na kuwa hadi sasa tayari ni miezi mitano na kwa mujibu wa mkataba bado miezi sita mradi ukabidhiwe, lakini inavyoonekana ni kuwa kampuni hiyo tayari ilishaonesha kushindwa kazi ambayo walishapewa ya ujenzi wa Chuo Cha Ualimu Ndala.

“ Mkandarasi hii serikali siyo ya kuichezea, mwaka mzima sasa bado mko asilimia ambazo haziridhishi pia hakuna kasi ya majengo na hakuna vibarua wanaoendelea na kazi, mnadeni Chuo Cha ualimu Ndala, na hapa tena kwenye ujenzi wa Chuo Cha VETA Geita kuna tatizo na hata mazingira ya kumpa huyu mkandarasi kazi, niwaonye watu wa Idara ya manunuzi pale Wizarani kuacha kutoa kazi kwa watu waliokuwa na uwezo,” anasema Waziri Ndalichako,

Waziri huyo yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa vyuo vya Ufundi stadi vya Geita na Chato.
Posted by MROKI On Friday, January 25, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo