Nafasi Ya Matangazo

January 02, 2018

Waombolezaji na wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari wa Uhuru FM, Justine Limonga, wakati ukiwasili Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa kabla ya kufanyika mazishi yake Makaburi ya Saku yaliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
 Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mwanahabari, Justine Limonga.
 Waombolezaji wakisubiri kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu kwenda eneo maalumu ilipo kufanyika ibada hiyo.
 Familia ya marehemu ikiwa kwenye ibada hiyo.
 Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani, ikitoa burudani.
 Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani,  Philo Mbunda, akitoa mahubiri.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Ibada ikiendelea
 Mwanamuziki Nguri, John Kitime akizungumzia jinsi alivyomfahamu marehemu Limonga.
 Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Moni Nyangasa, akizungumza kwenye ibada hiyo.
 Msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alfred Lucas, akizungumza kwenye ibada hiyo.
 Mbunge wa zamani wa Temeke, Abbas Mtemvu akimzungumzia marehemu Limonga.
 Mbunge wa Mbagala,  Issa Mangungu, akizungumza.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali, akizungumza katika ibada hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali, akiwapa pole wafiwa.
Mwanamuziki nguri, Hussein Jumbe, akiimba wimbo maalumu aliomtungia mwanahabari Justine Limonga.
*************
Dotto Mwaibale na Kulwa Mwaibale
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, ameongoza mamia ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanahabari, Justine Limonga iliyofanyika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam leo mchana.

Akizungumza katika ibada hiyo, Polepole alisema CCM na tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa bado akitegemewa.

"Tumempoteza mtu muhimu ambaye alikuwa akitegemewa kama chama tutaangalia namna ya kuisaidia familia yake," alisema Polepole.

Mkurugenzi wa Nduvini Auto Garage, Alhaji Ahmed Msangi alizungumza jinsi alivyomfahamu marehemu ambapo aliahidi kampuni yake kwa kipindi hiki cha kufunguliwa kwa shule itawanunulia vifaa vya shule, sare na kuwalipia karo wakati wakisubiri kukaa na familia kuona namna ya kuwazesha watoto hao kielimu.

Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali alisema kifo cha mwanahabari huyo aliyekuwa mwajiriwa wao kimeacha pengo kubwa ambalo halitazibika.

Alisema Limonga alikuwa mhariri na mbunifu na aliweza kuongoza vipindi mbalimbali ambavyo vilipendwa na wasikilizaji wa Uhuru FM ambapo aliahidi stahiki zote za marehemu kama mwajiriwa zitapatikana kwa wakati.

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, dini, siasa wanamuziki na wanahabari na wananchi iligubikwa na majonzi na baadhi ya watu kushindwa kujizuia kulia.

Akitoa mahubiri kwenye ibada hiyo Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani, Philo Mbunda alisema mwenzetu Limonga amemaliza kazi ya hapa duniani je sisi tuliobakia tumejiandaeje?

Mbunda alisema kila mtu anapaswa kujitafakari maisha yake ya kiroho kabla ya kifo na hivyo ndivyo Mungu wetu anavyohitaji.

Limonga alifariki dunia Desemba 30, mwaka jana katika Hospitali ya TMJ alikolazwa akitibiwa na ameacha mjane na watoto wawili ambapo mazishi yake yamefanyika leo katika Makaburi ya Saku yaliyopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, January 02, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo