Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde mwishoni mwa wiki amekabidhi matofali 3000 na mifuko ya saruji 100 katika Kata ya Makutupora kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Shule za Msingi Mpya za Mbande na Muungano Wilaya ya Dodoma mjini mkoani Dodoma.
Msaada huo alioukabidhi umetoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka ambayo ilikabidhi zawadi kwa washindi katika droo ya michezo hiyo,Mavunde aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza zaidi ili kusaidia kuboresha Elimu nchini.
Waziri
Mavunde alisema kuwa ujenzi wa shule hizo utasaidia kupunguza adha
inayowapata wanafunzi kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 7
kufuata shule katika eneo la Veyula.
"TATU MZUKA kwa ushirikiano na Naibu Waziri,
Kazi, Ajira na Vijana Mh. Anthony Mavunde (Mbunge Dodoma
Mjini) wakikabidhi matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa mmoja wa viongozi katika kata ya
Makutupora kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na
Mbande. Kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili kila moja.
"TATU MZUKA kwa ushirikiano na Naibu Waziri,
Kazi, Ajira na Vijana Mh. Anthony Mavunde (Mbunge Dodoma
Mjini) wakiwashukuru baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa kata ya
Makutopora mara baada ya kukabidhi matofali 3000 na mifuko 100 ya
saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na
Mbande.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoka kijiji cha
Makutopora na Mbande kushuhudia tukio la makabidhiano ya matofali 3000
na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za
Muungano na Mbande,iliyotolewa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya
Tatumzuka ikishirikiana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony
Mavunde.
0 comments:
Post a Comment