Nafasi Ya Matangazo

November 17, 2017

 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hossea Ndagala akinawa mikono ikiwa ni uhamasishaji jamii kutumia vibuyu chirizi vya kunawia mikono baada ya kutoka chooni.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
JUMLA ya kaya 35217  zimekaguliwa Wilayani Kakonko na kubaini asilimia 96.8% ndizo zinavyoo na asilimia 3.2% hazina vyoo na kati ya kaya hizo ni kaya 4231 ndizo zina vyoo bora sawa na 12% na asilimia mbili ya kaya hizo hunawa mikono baada ya kutoka chooni suala linalopelekea ongezeko la Magonjwa ya tumbo na kupoteza Nguvu kazi ya kufanya maendeleo katika  halmashauri hiyo .

Akitoa takwimu hizo katika zoezi la uhamasishwaji wa Utunzaji wa mazingira na ujenzi wa Vyoo bora na matumizi ya vibuyu chirizi kwaajili ya kunawia mikono baada ya kutoka chooni lililo andaliwa na shirika la TCRS jana Afisa  mazingira Wilayani humo,Nuhu Barakabitse alisema mpaka sasa muamko wa Wananchi wa wilaya hiyo ya matumizi ya vyoo bora ni mdogo sana hali inayoweza kupelekea ongezeko la magonjwa ya mlipuko.

Alisema Suala la maendeleo linaendana na uhifadhi na kuwa na Afya bora bila kuwa na Afya bora Wananchi hawawezi kufanya kazi pasipo kuwa na Afya njema, hivyo aliwaomba Wananchi kurndelea kuchimba vyoo bora na kuweka vibuyu chilizi katika maeneo yao ilikuepukana na Magonjwa hayo.

Hali hiyo imemlazimu Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala kuagiza viongozi wa serikali ya kijiji  Kata na tarafa kuwachukulia hatua walewote watakao shindwa kujenga vyoo bora ifikapo Mwisho mwa  mwezi wa kumi na mbili, ilikuepukana na Upungufu wa vyoo bora na ongezeko la magonjwa ya mlipuko na magonjwa yatokanayo na uchafu.

Kanali Ndagala alieleza kuwa hawawezi kuvumilia uzembe huo wakati wengine wenyewe wanazungumzia masuala ya vyoo jambo ambalo linatia aibu sana na linarudisha nyuma maendeleo ya Wananchi wa Wilaya ya Kakonko na kuwaagiza viongozi wa vijiji kumaliza kero hiyo na kuendelea na masuala mengine ya kuhimiza maendeleo.

"Ni fedheha kubwa  sana kwa kaya kukosa choo hivi wewe ni baba mwenye nyumba au Mama unaenda wapi? Au mnataka nani awajengee vyoo serikali au? Hii tabia ya kwenda vichakani iishe igike mahali wachukuliwe hatua wale wote ambao hawana vyoo waadhibiwe, sote tunajua umuhimu wa kutunza mazingira hatutafika mbali tuyatunze mazingira yatutunze", alisema Ndagala.

Kwa upande wake mraribu wa miradi ya maji, usafi wa Mazingira na ujengaji wa vyoo bora kutoka katika shirika la Norwegian Church aid actalliance  , Zakayo Makobero alisema mradi huo unashilikiana na Wananchi katika ukuaji wa maendeleo, kwa Wilaya hiyo mradi umetekelezwa katika vijiji vitano vya,kasongati, Kiga, Kiduduye , Itumbiko na  kiyobela kwa kujenga vyoo vyenye ubora kutoka asilimia 15% hadi kufikia asilimia 40% pamoja na kuhimiza unawaji mikono baada ya kutoka chooni na Wananchi wameendelea na utaratibu huo.

Alisema lengo la mradi huo ni kuhakikisha Wanahimiza wananchi wanakuwa na vyoo bora na kunawa mikono na sabuni pindi watokapo chooni ilikupunguza magonjwa yatokanayo na uchafu na kwa vijiji vitano vya Wilaya ya Kakonko wamefanikiwa kuchimba mashimo ya vyoo 184, kutoa mafunzo ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora kwa Walimu 35 na kuwapatia elimu wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji.
Posted by MROKI On Friday, November 17, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo