Meneja
wa Shamba la Kahawa, Aviv, linalomilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited lililoko
kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini Bw.Hamza Kassim,
(katikati), akizungumzia mradi wa umeme wa Makambako-Songea ambao utaunganishwa
kwenye kiwanda chake, mbele ya wahariri wa vyombo vya habari waliofika
kiwandani hapo ili kujionea manufaa yatokanayo na mradi huo katika uwekezaji
mkubwa, Oktoba 12, 2017.
Meneja
wa Shirika la Umeme Tanzania, 9TANESCO), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya,
(wakwanza kulia), akizungumza kwenye eneo la Shamba la Aviv, kuhusu hatua iliyofikiwa
na TANESCO kupeleka umeme wa kutosha kwenye shamba hilo ifikapo Desemba mwaka
huu wa 2017. Wengine pichani kutoka kushoto mstari wa mbele, ni pamoja na
Meneja Mradi wa umeme Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, na Meneja wa
Shamba hilo, Bw. Hamza Kassim, (katikati).
Na K-VIS Blog/Khalfan Said, Songea
UONGZI
wa Shamba la Kahawa la Aviv, lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45
kutoka
Songea mjini, umesema Mradi wa umeme wa Makambako-Songea utaleta nafuu
kubwa ya
kupunguza gharama za kuendesha majenereta ya kufua umeme kwenye shamba
hilo kwa asilimia 70, Meneja wa shamba Bw.Hamza Kassim amesema.
Akizungumza
na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea shamba hilo ili kupata
maoni ya wamiliki kuhusiana na mradi mkubwa wa umeme wa 220kV,
Makambako-
Songea Oktoba 12, 2017, Bw. Kassim alisemamahitaji ya umeme kwenye shamba hilo ni
Megawati 2.25 hadi 2.5 na zote hizo zinazalishwa na umeme wa kutumia
mafuta (Jenereta).
shamba
hilo linalo ilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited yenye makao yake
makuu nchini Songapo, lina ukubwa wa Hekta 1,012 kati ya hizo, Hekta
1,000,000 zimepandwa mazao.
“Mimea
ya Kahawa ambayo imefikia hatua ya kupevuka (matured), ni Hekta 800,
huku Hekta
200 bado ni Kahawa changa, tunatumia nishati ya umeme kwa shughuli za
umwagiliaji na ubanguaji wa Kahawa ambapo kwa siku tunatumia lita 4,000
za dizeli kuendesha jenereta hizo.” Alifafanua Bw. Kassim.
Ujio
wa mradi huu ni faraja kubwa kwetu na tunashukuru mradi huu
utakapokamilika utatupunguzia gharama za uendeshaji kwa asilimia 70 na
hivyo kutupa fursa ya kufanya upanuzi zaidi wa kilimo cha kahawa,
Alibainisha Meneja huyo.
Kwa
upande wake Meneja wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi
Patrick Lwesya alisema, Shamba la Aviv, ni moja kati ya wateja wake elfu kumi,
(10,000), ambao wataunganishiwa umeme,
Desemba mwaka huu 2017 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa usambazaji
umeme wa kilovolti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa ya
Songea na Njombe.
“Shamba
hili ndio wateja wetu wakubwa kabisa, na tunamuhakikishia muwekezaji huyu kumpatia umeme zaidi
endapo atauhitaji kwani kwa sasa tunazalisha umeme kwa asilimia 99.75, lakini
mradi ukikamilika tutazalisha kwa asilimia 100 na umeme utakuwa bora na wa
uhakika.” Alisema Mhandisi Lwesya.
Alisema,
pamoja na mteja huyo wa shamba la Kahawa la Aviv, pia wateja wengine
watakaofikishiwa umeme chini ya mradi huo ni pamoja na wale wa Mji wa Songea,
vijiji vilivyo katika wilaya za Mbinga, Namtumbo na Halmashauri ya Madaba.
“Nitoe
wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza mkoani kwetu kwani tunao umeme wa kutosha
kutokana na uzalishaji wake ambapo tunazalisha jumla ya Megawati 6.3 huku
mahitaji halisi ya Mkoa ni Megawati 5.3.” Alisema.
Hata
hivyo kumekuwepo vitendo vya uharibifu wa miundombinu hiyo mipya iliyojengwa
chini ya mradi huu vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wanaochoma misitu kwa
ajili hya kuandaa mashamba.
Wahariri
walishuhudia nguzo mbili moja ikiwa imeungua vibaya huku nyingine ikiwa
imeungua kabisa na kubaki nyaya zikining’inia kandokando ya barara ya
Songea-Mbinga kwenye kijiji cha Lipokela.
“Vitendo
hivi vinasikitisha sana, niwaombe wananchi waache tabia hiyo kwani mradi huu
unakwenda kubadilisha maisha yao na kwa kufanya uharibifu huu ni kuhujumu
jitihada za Shirika la Umeme TANESCO kwa niaba ya Serikali, kutatua changamoto
ya upatikanaji umeme wa uhakika kwa wananchi.” Alisema Meneja wa Mradi wa umeme
wa Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya.
Maneno
ya Meneja huyo yaliungwa mkono na Meneja wa Shamba la Aviv ambalo liko jirani
na eneo ambako nguzo hizo zilichomwa moto na kutaka utamaduni wa wananchi wa
mkoa wa Ruvuma wa kuchoma moto nyasi na misitu kwa nia ya kutayarisha maeneo ya
kilimo waache.
“Nilifurahi
ni hivi majuzi tu Mkuu wa Mkoa alizunguzia vitendo hivi na kuwaagiza viongozi
wa serikali kwenye kata na vijiji kuwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya
vitendo hivyo, na kwa uoande etu sisi tumejenga mifumo ya kuzima moto kuzunguka
eneo letu la shamba.” Alibainisha.
0 comments:
Post a Comment