Habari
njema zinatoka kwa nguli wa mavazi Afrika, Mustafa Hassanali, amekuwa mmoja
kati ya wabunifu 21 kutoka Afrika, ambao wameonesha vipaji vyao vya kipekee
katika jukwaa la mitindo lenye hadhi ya kipekee Afrika, linalofanyika kila
mwaka nchini Ethiopia lijulikanalo kama “HUB OF AFRICA FASHION WEEK 2017”.
Wiki
hii Mustafa alizindua mavazi yake mapya yaliyobeba jina la “tengeneza
Tanzania “ au “Make in Tanzania”.
Mavazi
hayo vyenye nia ya kutoa mchango katika kutimiza juhudi za Rais wetu, John Magufuli,
katika kutimiza sera uchumi wa viwanda na uwekezaji, na si hivyo tu bali,
kutoka kipindi hicho hadi leo, yamekuwamatamanio makubwa ya Mustafa kuanzisha
na kutangaza viwanda vya nguo vilivyopo Tanzania, na kufanya nchii yetu
kuwa soko pekee kwa nchi zingine za Afrika. Na hiyo ndo siri pekee ya mavazi
yake.
Mavazi
haya yamekuwa na utofauti kubwa na mavazi mengine ya Mustafa, “Make in Tanzania
Collection” ni nguo zenye mikato ya kipekee, na michoro ya kupendeza iliyopo
katika kitambaa hicho cha pamba.
Mavazi
hayo yamepambwa na mkusanyiko wa rangi nzuri na nguo hizi zinapendeza kuvaliwa
katika mitoko ya mchana au msimu wa kiaangazi na hufaa kwa wote wanaume na
wanawake.
Kama
Rais wa Marekani marehemu John F Kennedy alivyowai kusema “usiulize nchi yako
inaweza kukufanyia nini, uulize unachoweza kufanya kwa nchi yako”, hivyo basi
Mustafa haja tangaza jina lake tu pia amekuza na amepata nafasi ya kujulisha
wadau wa viwanda na wahamasishaji mitindo duniani, uwepo wa Viwanda vya nguo na
sekta ya Mitindo ya Tanzania kupitia ubunifu wake wa mitindo.
Mbunifu Mustafa Hassanali katika maonesho hayo.
Wanamitindo waki[pita kuonesha mavazi ya Mbunifu Mustafa Hassanali
0 comments:
Post a Comment