Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, Kanali
Hosea Ndagala, amewataka Wanafunzi wa kidato cha sita wa Oparation ya Tanzania ya Viwanda waliokuwa wa kihitimu
mafunzo yao katika Kambi ya Kanembwa KJ
824 Wilayani humo kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine.
Kanali Ndagala aliwataka wahitimu hao kuwa mfano
kwa Wenzao pindi watakapo kwenda vyuoni kwa kujiepusha na na vitendo vya anasa na
kila aina ya maovu katika jamii, kwakutumia taaluma na mafunzo waliyoyapata kwa
kujiajiri kwa maendeleo yao na taifa.
Aidha
Kanali Ndagala aliwaasa Vijana hao kuendeleza uzalendo na uwajibikaji
waliofundishwa na wakufunzi wao wa Jeshi la Wananchi kuwa wazalendo kwa
kufichua waovu na kukomesha vitendo vya uhalifu katika maeneo yao na kujiepusha
na matumizi ya madawa ya kulevya na zinaa ili Taifa liendelee kuwa na Vijana
Wenye nguvu na watakao saidia adhima ya serikali ya Tanzania ya Viwanda
kukamilika.
Vijana 954 waliohitimu mafunzo hayo kwa Mujibu
wa Sheria katika kambi hiyo, ambapo aliwataka
Vijana hao kujiepusha kutumiwa na makundi yasiyofaa na kufanya uhalifu
watakapo kwenda vyuoni na Wakawe mfano kwa Wenzao kwa kufanya mambo
yanayopendeza ikiwa ni pamoja na kujiajili kwa kuanzisha shughuli mbalimbali
kutokana na mafunzo waliyopatiwa.
Mkuu huyo
alisema lengo la serikali kuanzisha mafunzo hayo, ni kutaka Vijana kuwa na
uzalendo na kujifunza namna ya kujiajiri na kuacha kusuburi hadi serikali itoe
ajira na kuwafanya kupenda kufanya kazi na
kuondoa ubaguzi wa kikanda.
"Niwapongeze kwa kucheza gwaride zuri na
michezo mingi hii inaonyesha ni jinsi gani mlivyo iva katika mafunzo ya Jeshi
la Kujenga Taifa, niimani yangu
mtaisifia serikali kwa kushirikiana na jeshi la akiba kwani mafunzo haya ni ya
thamani sana na ni fursa ya pekee, kwani wapo wengi wangetamani kuwa kama ninyi
wamekosa na hivyo mtaitekeleza sera ya
uchumi wa viwanda kwa weledi mkubwa kutokana na mafunzo haya yamewajengea hali
ya kulipenda na kulitumikia taifa letu na yamewajengea umoja wa kindugu hii
itasaidia kuwa na taifa la amani, umoja , mshikamano na maendeleo",
alisema Kanali Ndagala.
Kanali Julius Kadawi kwa niiaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alisema
waasisi wa jeshi hilo waliamua kuanzisha
chombo kinacho husika kutoa malezi kwa vijana wa Tanzania waweze kuendana na
maadili ya makabila yetu vijana wasomi walijenga kasumba ya wao kuawa bora
kuliko waliosoma majukumu na melenga kuwajenga vijana kuwa na moyo wa uzalendo,
kujituma, kujiajili na kuipenda nchi yao na kujitoa kwaajili ya Nchi yao.
Akimkaribisha mgeni rasimi Mkuu wa kikosi cha
KJ824 Gerald Mollo alisema vijana wa Mujibu wa oparatini Tanzania ya
viwanda Walianza 979 wavulana wanne na msicha mmoja waliacha mafunzo kwaajili
ya ugojwa Wanafunzi wengine waliacha mafunzo baada ya utoro walipokwenda kujaza
gomu walitoroka vijana Waliohitimu mafunzo jana ni vijana 954 na ndio
walioshiriki katika kilimo cha umwagiliaji hekari 50 kambini, maandalizi ya
mashamba mapya hekari miamoja shughuli hizo walizifanya kutokana na elimu
waliyopo.
Nao Wanafunzi hao waliokuwa wakihitimu mafunzo
hayo waliiomba serikali kutofautisha muda wa mafunzo na kipindi cha udahiri
hali inayo wapelekea muda wa mafunzo kuwa mdogo na kushindwa kupata mafunzo
ipasavyo na kuwaomba Wanafunzi
wanaokimbia mafunzo hayo kuacha fikira potofu kwani mafunzo hayo yanawajenga
kiakili na kimaadili na kuwafanya kuwa bora sana.
0 comments:
Post a Comment