Mkurugenzi Mtendaji wa
Multichoice Tanzania Maharage Chande akielezea kuhusu msimu mpya wa Soka
ndani ya DStv wakati wa hafla maalum ya kuzindua kampeni ya msimu wa
Soka ijulikanayo kama
“Full vyenga Bila Chenga”. Katika hafla hiyo DStv ilitangaza kuwa
michezo mingi ya ligi ya Uingereza sasa itakuwa inarushwa kwa lugha ya
Kiswahili katika king’amuzi cha DStv. Kulia ni Leyla Patrick na kushoto
ni Robert Mgendera wakiwa wamevalia jezi za timu
mashuhuri za ligi ya Uingereza.
*******************
Wakati viguvugu la soka
ulimwenguni likizidi kupanda, rudimentary Kampuni ya Multichoice
Tanzania kupitia king’amuzi cha DStv imezindua kampeni maalum ya Msimu
mpya wa Soka ijulikanayo kama
‘Full vyenga Bila Chenga’ ambapo watanzania kupitia DStv wataweza
kushuhudia mubashara michuano mikubwa ya soka ulimwenguli inayotarajia
kuanza hivi karibuni ikiwemo Ligi kuu ya Uingereza (PL) na ligi ya
Hispania (La Liga) pamoja na makombe mengine maarufu
Duniani.
Pazia la ligi kuu ya
uingereza litafunguliwa jumapili Agosti 6 kwa mtanange wa ngao ya jamii
kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaonyeshwa mubashara kupitia
DStv.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika ofisi za Multichoice
Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice
Tanzania Maharage Chande
amesema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote
kuliona soka katika muonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia
michuano hiyo kwa matangazo yatakayorushwa kwa lugha ya Kiswahili.
“Msimu huu watanzania,
kupitia DStv, siyo tu kwamba wataona michuano mbalimbali ya soka
ulimwenguni mubashara, bali pia watayaona katika ubora wa hali ya juu
yaani High Definition na zaidi
ya yote, tutawapatia fursa watanzania kufuatilia ligi kuu ya Uingereza
kwa lugha ya Kiswahili”.
Amesema DStv imeendelea
kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vipindi na kurekebisha bei za
vifurushi ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya
kujionea matukio mbalimbali
muhimu katika Nyanja zote za maisha ikiwemo michezo na burudani. Ametoa
mfano wa ligi ya Hispania La Liga ambayo inaonekana yote katika
kifurushi cha Bomba. Pia baadhi ya mechi za ligi kuu ya Uingereza (PL)
pia zitaonekana katika kifurushi cha Bomba.
Kwa upande wake, Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria amesema kampeni ya Full Vyenga
bila Chenga inamaanisha kuwa wateja wa DStv, msimu huu wa soka wataweza
kuliona soka kwa
muonekano bora zaidi, yaani bila chenga. “Tunatambua kuwa washabiki wa
soka sasa wanataka walione soka vyema, kana kwamba nao wapo uwanjani.
Kwa DStv, sasa hata mtu akilambwa chenga utaiona vyema, hata kama mtu
anatoka jasho utaliona. Hakuna wingu wala ukungu,
ni ‘full vyenga bila chenga’ alisema Alpha.
0 comments:
Post a Comment