Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na
Wanariadha wenzake Nelson Mbuya (wa pili kushoto), Stephano Huche na
Joseph Panga(kulia)
wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka
mjini Arusha hadi wilayani Monduli. Wanariadha mbalimbali wameweka
kambi jijini Arusha ikiwemo timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki
mashindano ya riadha ya dunia. Jumla yawanariadha
7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao
wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini
London
Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na Wanariadha
wenzake Nelson Mbuya (katikati) na Joseph Panga wakiwa katika mazoezi
makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi
wilayani Monduli. Wanariadha mbalimbali wameweka kambi jijini Arusha
ikiwemo timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya riadha ya
dunia. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki
mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano
hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London
Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana (Kushoto)
akimkabidhi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce Simbu (Kulia)
wakati wa ziara ya afisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya taif
ya riadha inayojiandaa kushieiki mashindano ya riadha ya Dunia
yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni kocha
Francis John na mwanariadha Sara Ramadhani. Jumla yawanariadha
7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao
wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini
London
Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na Wanariadha
wenzake wa timu ya taifa itakayoshiriki Mashindano ya Riadha ya Dunia
jijini London wiki ijayo Ezekiel Ng’imba (katikati) na Said Makula
wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka
mjini Arusha hadi wilayani Monduli. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa
kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao
wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini
London.
***************
Balozi
maalum wa DStv na moja ya wanariadha wanaounda timu ya taifa
itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia ya mwaka huu
yatakayofanyika mwei ujao jijini London Alphonce Simbu, amesema
watanzania watarajie medali kutoka kwa timu hiyo kwani imejiandaa vizuri
Akizunngumza
wakati wa ziara maalum ya Afisa muandamizi wa DStv Johnson Mshana
katika kambi hiyo iliyopi Ilboru Arusha ambapo pia alishuhudia mazoezi
ya timu hiyo, Simbu alisema kuwa yeye na wenzake wamejiandaa kikamilifu
kuhakikisha kuwa wanaleta medali nyumbani katika
mashindano hayo makubwa yanayofanyika mapema mwezi Agosti.
“Tumejiandaa
vizuri na tunamatumaini makubwa ya kushinda. Tumekuwa tukifanya mazoezi
mazito na inaonekana vijana tuko sawasawa kupambana katika mashindano
hayo” alisema Simbu
Naye
meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana ambayo
alitembelea kambi hiyo na kasha kushiriki katika mazoezi amesema Kampuni
yao imefurahishwa sana na mwenendo wa kambi hiyo pamoja na timu nzima.
“Wakati wote tunapoamua kusaidia katika maandalizi
ya timu tunafahamu fika kuwa timu yoyote bila ya maandalizi ya kutosha
haiwezi kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote yale. Hii niyo sababu
iliyotusukuma DStv kusaidia katika juhudi hizi za kuiandaa timu yetu ya
Taifa itakayokwenda kuwakilisha nchi katika
mashindano ya dunia. Tunataka Watanzania tushuhudie medali zikija
nyumbani”
Amesema
baada ya DStv kuanza kumdhamini Simbu takriban mwaka mmoja uliopita,
wameshuhudia mafanikio makubwa sana. Ambayo yamewatia moyo sana kuamua
kuongeza nguvu ili kuiimarisha zaidi timu ili hatimaye iweze kufanya
vizuri zaidi na kulikwakilisha vyema taifa kwenye
michuano ya kimataifa.
“Tulianza
na Simbu, amefanya vizuri, ameshinda, sasa tunaongeza wigo wa ushindi
kwa timu yetu ya Tanzania na tunaamini tutashinda, mbali na hayo DStv
ilionyesha mubashara Mumbai Marathon tukamuona Simbu akishinda,
Tukaonyesha Mubashara London Marathon, tukaona Simbu
akivunja rekodi yake, na tutaonyesha mubashara Mashindano ya Dunia
Mwezi Agosti, ambapo bila shaka kwa nguvu hii, tutashuhudia tukikwapua
medali kedekede na kuliletea taifa letu sifa kubwa” alisema Mshana kwa
kujiamini
Naye
Kocha wa timu hiyo Francis John, amesema kazi kubwa imefanywa na makocho wanaoinoa timu hiyo hapo kambini na kwama
ushirikiano mkubwa kati ya makocha na wachezaji umefanya mazoezi
yao kwenda vizuri. Amesema wanatarajia kuwa wanariadha hao watafanya
vizuri
kwani hata mmoja wao aliyekuwa na matatizo ya magoti sasa anaendelea vizuri na bila shaka atasiriki vizuri kwenye mashindano.
Amesema
jumla ya wachezaji saba wakiwemo wanawake watatu na wanaume wane watashiriki Failuna Abdi
atashiriki mita 10,000 Gabriel Gerald mita 5,000 na
watano watashiriki marathon kamili ya kilomita 42 ambao ni
Magdalena Krispin, Saraah Ramadhani, Said Makula, Ezekiel Jafar Ng’imba
na Alphonce Felix Simbu.
Timu
ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo inatarajiwa kuagwa na
kukabidhiwa bendera jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai na Mashindano
hayo yanaanza tarehe 4 Agosti 2017.
0 comments:
Post a Comment