Kamishna Mkuu wa TRA nchini,Charles Kichere, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akizungumza.
Na Atley Kuni- Afisa habari
Mwanza.
Mamlaka
ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia
Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha
wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.
Kauli
hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini, Charles Kichere, alipokuwa
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.
“Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila
adhabu ni Juni 30, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza
(Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu
nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za
mitaa yao au kujisajili na kulipa
kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere.
Kichere
amefafanuakuwa kwa walioko
sehemu ambazo nyumba zi methaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani
ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo
hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na
mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.
Kichere amevitaja viwango hivyo
vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na
kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela.
TRA
pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa
Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia
viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii,
kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha
uthamini wa majengo” amesema Kichere.
Kwa
Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma
hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo
hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha
wa 2016/2017.
“Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie
tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi
labda kama amepata Msiba” amesema Mongella.
Akijibu maswali ya waandishi wa
habari waliotaka kujua ni kwa namna gani TRA inaweza kufanya ili
kurahisisha mfumo wa malipo kwakutumia mitandao ya simu, amesema wao kama TRA
kila siku hupokea maoni ya wadau ili kuboresha shughuli zao na kwa hali hiyo
wanaona ni wazo jema.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA,
pamoja na majukumu yake imeongezewa jukumu lakukusanya kodi za majengo ambapo
mara baada yakukusanya kodi hizo, zitatolewa taarifa, lakini pia
zitapelekwa kwenye Halmashauri husika kwa ajili ya shughuli za
Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment