Na Bety Alex, Arusha
Chama cha mawakili Tanganyika
TLS kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa urais wa chama hicho kesho ambapo hadi
sasa wagombea watano wamejitokeza kugombea
nafasi hiyo.
Akizungumza katika mkutano
mkuu wa chama hicho unaoendelea jijini Arusha
rais mstaafu anayemaliza muda wake John Seka amesema uchaguzi wa
mwaka huu umekua na hamasa kwakuwa
umehusisha wagombea ambao wanafahamika zaidi na jamii na pia umefanyika kwenye
sheria mpya za
uchaguzi wa chama.
Seka amewataja wagombea hao
maarufu kuwa ni Tundu Lisu,Fransis Stola,Laurence Masha,Victoroia Mandarin na
Godwin Mwapongo.
Aidha Seka amewataka
wanasheria kuzingatia misingi ikiwa ni pamoja na kuisaidia na kuishauri serikali katika utungaji wa sheria za bunge
na mahakama na ili kuongeza nguvu
katika kuwasaidia wanyonge na wasio na
uwezo waweze kupata haki.
Amewataka wanachama wa chama
hicho kujitathimini ni kiongozi gani atakayefaa kupigiwa kura ili aweze
kukabidhiwa kijiti cha kuongoza chama hicho.
Kwa upande wake wakili wa kujitegemea
dr Eva Hawa Sanare amewataka wanasheria
kusoma sheria mpya ya katiba ya Kenya
low society kwa kuwa wanasheria bado
hawajaelewa utawala wa sharia Wajiendeleze ili
kuepuka kesi ambazo hazijakamilika kwani baadhi yao wamekuwa wakiendesh
akesi ambazo hazijakamilika Amesema kuwa
bila wanasheria kufanya kazi yao na kuielewa kwa undani hawataweza kuendeleza
majukumu yao ya kuisaidia jamii
0 comments:
Post a Comment