Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya
Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Bodi ya
Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ikiwa ni
sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye Hotel ya Hyatt Kempinsk
The Kilimanjaro Dar es Salaam leo. Kikwete ni Mwenyekiti wa Taasisi
hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Jakaya
Kikwete, alisema kuwa Taasisi hiyo pamoja na mambo mengine itajihusisha
na masuala ya Maendeleo ya Binadamu nchini, Afrika na Duniani.
Na.
Immaculate Makilika- MAELEZO
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa anapenda
kuendelea kufanya shughuli zinazosaidia kuleta maendeleo kwa watu na jamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa
akizindua Taasisi yake ya Jakaya Kikwete (Jakaya Mrisho Kikwete
Foundation) alisema kuwa kwa muda mrefu amekua akipenda na kujihusisha na
shughuli mbalimbali za maendeleo ya watu na hivyo Taasisi yake itamsaidia
katika kufikia malengo yake.
“Nimetumia
muda wangu kwa ajili ya maendeleo ya watu, baada ya shule, nilikitumikia Chama
cha Mapinduzi(CCM), nilitumikia Jeshi na baadae Serikali, kwangu Taasisi hii
imekuwa chombo kitakachonisaidia kuendeleza maono yangu na kutimiza ndoto zangu
katika kuendelea kusaidia watu” alisema Dkt. Kikwete. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Akiizungumzia
taasisi hiyo Kikwete alisema kuwa, Taasisi yake ina wajumbe 9 kutoka sehemu
mbalimbali duniani wenye nyadhifa na heshima kubwa katika nchi zao.
Ameongeza
kuwa Taasisi hiyo imejikita kusaidia jamii katika maeneo makubwa manne,
maendeleo ya jamii hasa katika kujikita kuondoa umaskini, mabadiliko ya
hali ya nchi na kilimo kwa wakulima wadogo.
Pia
Taasisi hiyo imejikita katika huduma za afya, kutokomeza malaria na afya ya
mama na mtoto.
Maeneo
mengine ambayo Taasisi hiyo inajihusisha nayo ni ni elimu kwa
vijana ili kukuza vipaji vyao na kuwapa mafunzo kuhusu uongozi
bora, usawa wa kijinsia na namna ambavyo Serikali inavyotoa huduma kwa wananchi.
Aidha,
alisisitiza kuwa Taasisi yake itaisaidia Serikali, mashirika na Taasisi
mbalimbali ili kushirikiana kuwaletea maendeleo watanzania na watu mbalimbali
duniani.
Dkt.
Kikwete amewataja Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi yake kuwa ni Balozi
Ombeni Sefue aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Profesa Rwekaza Mukandala Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Willium Mahalu Mhadhiri
Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Tabibu cha Bugando.
Wengine ni
Balozi Mwanaidi Maajar aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,
Abubakar Bakhresa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa,
Genevieve Sangudi Mtaalamu wa Masuala ya kibishara ya Kimataifa kutoka
Marekani.
Pia
wapo Dato’ Sri Idris Jala, Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu nchini
Malyasia, Balozi Charles R. Stith aliyekuwa Balozi wa zamani wa Marekani
nchini Tanzania pamoja na Dkt. Carlos Lopes ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Taaisi ya Mafunzo na Utafiti ya Umoja wa Mataifa (UNITAR).
Taasisi ya
Maendeleo ya Jakaya Kikwete ilisajiliwa tarehe 17, Februari 2017, na hii ni
mara ya kwanza kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini kukutana tangu kuanzishwa
kwake.
Kikwete akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi yake ya JMKF
Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF,
Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo, Mfanyabiashara
maarufu Mtanzania aishie Marekani, Genevieve Sangudi
Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF,
Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo ya Wadhamini , Dato'
Sri Idris Jala, Waziri asiye na Wizara Maalumu Ofisi ya Waziri Mkuu wa
Malaysia na Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Pamendu)
nchini humo.
0 comments:
Post a Comment