Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akisheheresha kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya radio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues akitoa neno la ukaribisho liliombatana na ujumbe maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi Waziri Nape Nnauye (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiteta jambo na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues (katikati) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akimpongeza Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA) Prosper Kwigize kwa hotuba nzuri wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka na kulia ni Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi akizungumza kuhusu taratibu na sheria za utoaji leseni kwa redio za jamii nchini wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dk. Ayoub Rioba akifafanua jambo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Meneja wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika akitoa neno la shukrani wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (wa pili kulia) akimpongeza Meneja wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika baada ya kuwasilisha risala ya mafunzo ya ufundi kwa Redio za Jamii wakati maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam jana. Kulia Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi, Wa tatu kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Wanne kulia Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka na Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Washiriki kutoka redio za jamii nchini na waandishi wa habari waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Cho Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi akiwasilisha mada kuhusu upashanaji wa vyombo vya habari na sheria wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyoratibiwa na UNESCO na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, Rogers Dhliwayo akizungumza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) na namna radio inavyowezesha hamasa ya utekelezaji wake kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyoratibiwa na UNESCO na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Meza kuu kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa redio za jamii nchini wakati sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye(katikati) na meza kuu katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya COMNETA wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye(katikati) na meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa UNESCO Dar Luiana Temba (kushoto) na Rose Mwalongo Mataifa wakifurahi jambo kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
SERIKALI imewataka wanahabari kusoma sheria, taratibu na kanuni zinaogusa tasnia yao ili iweze kuendelea na kuachana na kuamini kila kitu wanachoambiwa na mtu mmoja.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati akizungumza katika siku ya radio duniani, hafla iliyofanyika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.
"Watu someni sheria, taratibu na kanuni kwa kina ili kujua na kuzielewa, mkielewa kama kuna sheria inakwaza ukuaji wa sekta ya habari tuseme tukae chini.. " alisema Waziri Nape akijibu hoja kuhusu sheria za habari zilizopo ambazo zinadaiwa kukwaza uhuru wa ukusanyaji wa habari.
Ilielezwa katika hafla hiyo kuwa sheria za sasa ya takwimu na habari zinakwaza uhuru wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Katika hoja hiyo Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA) Prosper Kwigize katika hotuba yake kwa Serikali, alisema kwamba redio hizo zinachangamoto nyingi katika utendaji wake ikiwamo sheria zilizopo,watoa habari wasioeleweka na wanazuia upatikanaji wa habari.
Nape alisema kwamba sheria si msaafu na kwa kuwa asilimia 80 za habari zinazalishwa na serikali, waandishi wanahaki ya kupata habari hizo na kama kuna kikwazo ni lazima kitafutiwe suluhu.
"Tukae tushindane kwa hoja tukubaliane na kuhakikisha kwamba tunarekebisha.. Bunge kazi yake ni kutunga na kufuta sheria" alisema Nape ambaye alisema kwamba sheria ya sasa imetoa nguvu kwa watoa habari na kwamba si kila habari iliyopo serikalini ni classified.
Alisema pia ili kufanikisha upatikanaji wa habari maofisa habari wamepewa maagizo ya kushiriki vikao ili waweze kutoa taarifa bila woga na kwa ujasiri mkubwa.
Alisema ni kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kukua kwa tasnia ya habari na itaendelea kupigania hilo kwa kuwa inatambua umuhimu wa vyombo vya habari.
Pamoja na kuweka mazingira mazuri amewataka wanaoendesha redio za jamii kutafuta namna ya kujiunga na taarifa za kitaifa (habari) ili wananchi wasitengwe na matukio ya maeneo mengine.
Alisema kwa kuwa sehemu kubwa ya redio hizo ziko pembezoni ni vyema nguvu yake ikatumika pia kuhabarisha matukio ya kitaifa.
Akizungumzia dawa za kulevya, Waziri Nape alitaka wanahabari kuwa na uzalendo na kushiriki katika vita hiyo kwa kutumia vyombo vyao vyote.
Alisema ni vyema wananchi na wanahabari wakatambua kwamba vita hiyo ni yetu sote na kwamba wanahabari wanauwezo wa kuunganisha wananchi katika kushinda hiyo vita ambayo ni kubwa.
Akizungumzia redio alitaka watu wanaotumia vyombo hivyo kuangalia namna ya kutoachwa nyuma wakati huu wa mabadiliko makubwa ya teknolojia na sayansi ambapo matumizi ya mtandao ya utoaji wa habari papo hapo unaendelea.
Aliwataka watu kuzungumza nafasi ya radio katika kuleta maendeleo huku wakiangalia changamoto zinazoletwa na teknolojia ya habari.
Sherehe hizo ambazo ziliambatanishwa na midahalo kuhusu upashanaji wa vyombo vya habari na sheria iliwasilishwa na Mkurugenzi wa utangazaji wa TCRA Ntobi na pia watendaji wa UNDP kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na namna radio inavyowezesha hamasa ya utekelezaji iliratibiwa na UNESCO.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues alisema akimkaribisha Waziri Nape kwamba washiriki katika sekta ya utangazaji wanatakiwa kuwa pamoja ili kukuza upashanaji wa habari katika maeneo ya pembezoni.
Alishauri kuwepo na kuaminiana ili kufanikisha malengo ya kuleta maendeleo kwa kupeana nafasi na kushirikishana.
Alitaka watanzania kutumia nguvu ya radio kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kitaifa na kuleta maendeleo yanayotakiwa.
Kukiwa na vituo vya radio 44,000 duniani Mwakilishi huyo wa UNESCO alisema kwamba radio bado ina maslahi makubwa kwa wananchi kutokana na kutoa sauti kwa wakazi ili kukabiliana na changamoto zilizopo.
0 comments:
Post a Comment