Na Pamela Mollel,Arusha
Imeelezwa kuwa
siku ya sheria ni siku ambayo wananchi wanapata fursa ya kupata msaada
wa kisheria ambayo kila mwananchi anapaswa kuwa chini ya shieria na sio
juu ya sheria.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake wakili wa kujitegemea Mruma Shabibu
kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku hii ni maalum kwa mawakili
kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.
Alisema kuwa kwa
siku hii watu wengi ufaidika kwa kutatuliwa baadhi ya matatizo yao bila
kutozwa gharama yeyote ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya kisheria
sanjari na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na mawakili.
Alidai kuwa
wananchi wanapaswa kuheshimu katiba lakini pia na kukaa chini ya sheria
ili haki iweze kutendekea kwani baadhi ya wananchi wanakaa juu ya sheria
hali ambayo inawafanya kujiona hawatendewi haki.
Hata hivyo
alifafanua kuwa lengo la kuanzishwa kwa siku hii ni kuangalia umuhimu wa
sheria katika jamii na kuona jinsi inavyofanya kazi katika kukuza
uchumi wa nchi
.Picha Wakili wa kujitegemea Mruma aShabibu
kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku hii ni maalum kwa mawakili
kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.
0 comments:
Post a Comment