Shirika la ndege la
kitanzania Precision Air limefanikiwa kufaulu kwa mara nyingine ukaguzi wa IOSA
na kupata cheti cha Usalama (IOSA)
kitolewacho na shirikisho la kibiashara la mashirika ya ndege duniani (IATA).
Precision Air imepata cheti hicho ikiwa ni kwa mara ya sita mfululizo (2006,
2008, 2010 na 2012, 2014 na 2016)
Mafanikio haya yamepatikana
baada ya kufanyiwa uhakiki wa usalama ambao hufanyika kila baada ya miaka
miwili. IOSA ni mkakati utambulikao na kukubalika kimataifa kwa ukaguzi wa utawala na usimamizi
wa shughuli za mashirika ya ndege katika maswala ya usalama.
Cheti hicho hutolewa
kama ishara ya shirika kukaguliwa na kufuzu kuwa na viwango vinavyo kubalika
kimataifa. Cheti cha sasa kitadumu kwa miaka miwili hadi Tarehe 22 Septemba
2018 ambapo Precision Air itafanyiwa ukaguzi tena.
Akizungumzia mafanikio
hayo Mkurugenzi mtendaji wa Precision Air Bi.Sauda Rajab, amesema Precision Air
imejizatiti na kuhakikisha inatoa huduma za uhakika na salama kwa wateja wake
na kwamba sikuzote usalama wa abiria na ndege
ni kipaumbele cha kwanza kwa shirika.
“Kupatikana kwa cheti
hiki kwa mara nyingine kuna maana kubwa kwetu sisi kama shirika na sekta ya
anga kwa ujumla, ni uthibitisho wa kiwango cha ubora wa huduma za usafri wa
anga kinachotolewa na shirika la kitanzania.” Ameongeza Bi.Rajab
IATA ni shirikisho la
kibiashara la kimataifa la mashirika ya ndege linalowakilisha mashirika zaidi
ya 240 yanayosafirisha zaidi ya asilimia 84% ya wasafiri wa anga duniani.
Shughuli za IATA zinasaidia uundwaji wa sera za mambo muhimu katika sekta ya
anga pamoja na maendeleo ya sekta hiyo katika nyanja ya usalama.
Shirika
la ndege la Precision Air ndilo shirika pekee la kitanzania lenye cheti cha
IOSA na mwanachama pekee wa shirika hilo kwa sasa. Precision Air inafanya
safari zake kutokea Dar es Salaam ambapo ndipo makao makuu yake kwenda
Mwanza,Arusha,Kilimanjaro,Bukoba, Musoma, Kigoma,Tabora,Mtwara, Zanzibar na
Nairobi.
0 comments:
Post a Comment