Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ametuma salamu za
pongezi kwa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa vijana wenye chini ya umri wa
miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kufuzu Fainali za Mashindano ya Africa kwa vijana
chini ya umri wa miaka 17.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa miguu
barani Afrika (CAF) imeeleza kuwa Serengeti Boys inafuzu fainali hizo mara
baada ya kushinda kwa rufaa yao dhidi ya Timu ya Congo Brazaville ambapo timu
hiyo ilimchezesha mchezaji Langa Lese aliyezidi umri wa miaka 17.
Mhe. Nape
amesema kuwa, hiyo ni fursa kubwa ambayo Tanzania imeipata katika mashindano ya
kimataifa na kuna kila uwezo na sababu ya kushinda na kuchukua kombe hilo.
Waziri
Nape ametoa shukrani zake za dhati kwa watanzania na wadau wa michezo kwa
michango yao ya hali na mali iliyoifanya Serengeti Boys kufikia hapa ilipofika na
kuzidi kuendelea kuiunga mkono kwa hali na mali timu hiyo katika kuelekea fainali
hizo.
Mhe. Nape
Moses Nnauye amewatakia mafanikio Serengeti Boys kuelekea katika Fainali za michuano
ya AFCON zitakazofanyika nchini Gabon Aprili, 2017.
0 comments:
Post a Comment