Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF)Dk. Reginald Mengi akizungumza jijini Dar es salaam jana wakati akitolea ufafanuzi juu ya baraza la kibiasha baina ya Uturuki na Tanzania lililoundwa juzi baaina ya taasisi hiyo na Bpodi ya mahusiano ya kigeni kwenye masuala ya kiuchumi nchini Utururuki (DIeK). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye (kushoto) akizungumzia uundwaji huo wa baraza la kibiashara baina ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Mwenyekiti wa TPSF ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF)Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana juu ya baraza la kibiasha baina ya Uturuki na Tanzania lililoundwa juzi baaina ya taasisi hiyo na Bpodi ya mahusiano ya kigeni kwenye masuala ya kiuchumi nchini Utururuki (DIeK).
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akifafanua jambo.
*************
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ni
chombo kilichoundwa mwaka 1998 kwa lengo la kuunganisha asasi za sekta binafsi
nchini kwa lengo la kujenga uchumi imara wa taifa kupitia sekta binafsi.
Bodi ya mahusiano ya kigeni kwenye masuala
kiuchumi nchini Uturuki (DIeK) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)
wameingia makubaliano kuanzisha Baraza la Kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
makubaliano haya yalifikiwa tarehe 23 Januari 2017, Dar es Salaam.
Baraza litakuwa na majukumu na shughuli
zifuatazo:
· Kusaidia kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili
·Kutoa mchango katika kuanzisha na kukuza viwanda,
kupitia ushirikiano wa teknolojia wa mashirika na taasisi za kiuchumi za nchini
uturuki.
·Kuratibu juhudi za pamoja kukusanya, kuunganisha,
kuchambua, kutathmini na kueneza taarifa zinazohusu biashara, viwanda na
masuala ya ushiriakiano kwenye teknolojia na uwekezaji; kwa nia ya manufaa ya
nchi zote mbili.
·Kutambua
changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo mbili na kwenye ushirikiano kiuchumi na kuleta
mapendekezo ya jinsi gani serikali husika zitakavyo zitatua.
·Kuwasilisha misaada katika kuandaa maonyesho
ya kibiashara na kuhamasisha wanachama wa baraza la kibiashara kushiriki kikamilifu
katika shughuli za namna hizo.
·Kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati(SMEs)
pamoja kuwapa ujuzi na maarifa.
·Kukusnya takwimu na taarifa juu ya fursa katika
biashara, uwekezaji na masuala mengine katika ushirikiano kiuchumi, na kusambaza
taarifa hii kwa wanachama.
Baraza la kibiashara baina ya Uturuki na
Tanzania litagawa katika kamati za kitaifa mbili. Kila kundi litakuwa na
wanachama wake na taasisi za kiuchumi au za kibiashara. DEiK itaunda sekretariat
ya upande wa Uturuki, na TPSF itaunda sekretariat kwa upande wa Tanzania.
Baraza kuu la biashara litahushisha sekta
mbalimbali za nchi hizo mbili na kuendelea kuangalia uwezekano wa ushirikiano
zaidi kwa manufaa ya nchi zetu mbili.
Kamati hizi ndogo za Baraza zinatarajiwa
kukutana angalau mara moja kwa mwaka, kutazama na kujadili mafanikio ya Baraza
kwenye masuala ya kibiashara, uwekezaji,teknolojia baina ya Utruki na Tanzania.
0 comments:
Post a Comment