Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza
mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.
Katibu Mkuu uyo aitoa
wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli
ya Sea Cliff ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini
William Mkapa alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na
kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya
wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo
jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina
mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza
kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa
kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo
upigaji marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga
pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.
Mbali na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua
wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika
biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.
Naye Rais Mstaafu wa awamu ya tatu
Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka watanzania kulinda na kutunza mbuga zetu
kwani ni urithi wa kila mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika
kulinda urithi huu wa wanyama na kuvitaka vyombo vya habari kushiriki vyema
katika kutangaza mbuga zetu na pia kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali
katika kutokomeza ujangili wa pembe za ndovu.
0 comments:
Post a Comment