Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi Simu ya Mkononi mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya
wakusanya taarifa za Bei za Mazao ya kilimo na Bidhaa Nyingine ikiwa ni
kitendea kazi kitakachowasaidia wakusanya taarifa.
Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa tatu kulia)
walioketi kwenye viti akiwa na picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya
Ukusanyaji wa Taarifa za Bei za Mazao ya Kilimo na Bidhaa Nyingine
yanayofanyika Mkoani Dodoma.Wa Pili (Kulia) walioketi ni Bw. Odilo Majengo Mkurugenzi
Idara ya Uhamasishaji Biashara na Bi. Hilda Mwampeta Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Uhamasishaji Biashara na Masoko Wizara
ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji.
********************
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
(WVBU) Prof. Adolf Mkenda amehitimisha mafunzo
ya ukusanyaji wa taarifa za bei za mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kwa
kukabidhi simu za Mkononi Washiriki wa Mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali
Tanzania bara.
Mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani hapa kwa siku nne
mfululizo na kuwashirikisha wakusanya taarifa wapatao 113 ngazi ya wilaya na
mikoa.
Katika Hotuba yake ya ufunguzi alieleza malengo ya
Mafunzo hayo kuwa ni kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa weledi zaidi kwa kuzingatia
maendeleo ya kiteknologia na Habari kadiri mahitaji ya taarifa yanavyoongezeka.
“mafunzo haya mnayopatiwa yanalenga kuwawezesha kukusanya
na kutuma taarifa za masoko ya mazao ya Kilimo pamoja na bidhaa nyingine kwa
wakati na usahihi Zaidi”.
Alisisitiza kuwa taarifa sahihi zitasaidia wakulima,wafanyabiashara,
watunga sera na Taasisi nyingine kufanya
mamuzi ili kuleta mageuzi ya kiuchumi yatakayoongozwa na uchumi wa Viwanda.
“Ni matumani yangu kuwa mtatumia weledi wenu na uzalendo
kuwapatia wakulima, wasindikaji au wenye viwanda na walaji taarifa sahihi
watakazozitumia katika kuendesha shughuli za kibiashara”.
Aliongeza kuwa taarifa sahihi na kwa wakati utasaidia kuondoa
utitiri wa madalali ambao hutumia mwanya wa ukosefu wa taarifa kuwanyonya wakulima kwa kutumia mbinu mbalimbali kama
vile kwenda moja kwa moja kwa wakulima na kununua mazao kwa wakulima badala ya kusubiri mazao yafike
sokoni.
Mafunzo haya yaliandaliwa na Wizara ya Viwanda na
Biashara kwa kupitia Mradi wa SECO UN
TRADE, pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) .
0 comments:
Post a Comment