NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
CHINA imesema, itajenga viwanda kuunga
mkono mkakati wa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais,
Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo Januari 9,
2017, na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Bw. Wang Yi, (pichani juu,
alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Bw. Kassim Majaliwa, kwenye makazi
yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ambaye amewasili leo mchana
akitokea nchini Zambia, alimuhakikishia waziri mkuu azma ya serikali ya
China, kujenga ushirikiano wa kihistoria baina ya mataifa hayo mawili.
Ziara ya Waziri huyo ambayo ni ya kufungua msimu mpya wa mwaka 2017 wa
uhusioano baina ya China na mataifa ya Kiafrika, inalenga kuweka
msisitizo wa ahadi alizotoa Rais wa China, alipotembelea Tanzania
mwishoni mwa mwaka jana.
Baadaye waziri huyo na ujumbe wake,
walikutana na kufanya mazunhumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mmabo ya
Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt.
Augustine Mahiga, kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius
Nyerere.
Waziri Mkuu, Bw. Kassim Majaliwa,
(kulia), akiwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa China, Bw.
Wang Yi, (wapili kulia), nyumbani kwake Oyseterbay jijini Dar es Salaam,
Januari 9, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Wang na ujumbe wake (kushoto),
wakifanya mazungumzo ya kiserikali na mwenyeji wake na Dkt. Augustine
Mahiga na ujumbe wake kulia, kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri Wanga, na mwenyeji wake, Dkt.
Augustine Mahiga, wakiwa kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari
baada ya mazungumzo ya kiserikali
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga,
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
Waziri Wanga Yi, na mwenyeji wake, Dkt. Mahiga, wakipiga picha rasmi
Waziri Wanga na mwenyeji wake, katika mkutano na wanahabari
Waziri Wanga, na mwenyeji wake, Waziri Dkt. Mahiga, wakitoka kwenye mkutano na wanahabari
Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Dkt. LU Youqing
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya
serikali wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (kushoto), akiongoza mkutano na
waandishi wa habari, uliohutubiwa na Mawaziri Wanga, na Balozi Dkt.
Mahiga
0 comments:
Post a Comment