Mkurugenzi
wa Legal Services Facility ,Scholastica
Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf
Wajumbe wa Bodi wa Legal Services Facility katika picha ya pamoja
Mwenyekiti wa bodi ya Lsf , Joaquine De Mello akiakabidhi hundi kwa mmoja wa wanufaika.
Mnufaika wa Ruzuku kutoka tasisi ya TEWORECakinyoosha hundi yake juu yenye thamani ya shilingi bilioni moja
Wanufaika wa Ruzuku wakiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa bodi
Mkurugenzi
wa Legal Services Facility ,Scholastica
Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf
Mkurugenzi
wa Legal Services Facility ,Scholastica
Julu, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa LSf
Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
WITO
umetolewa kwa wadau wa sheria kusaidia kupunguza
mahabusu Magerezani kutokana na wingi wao ambao aikuwa lazima kuwekwa humo .
Wito huo
umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la
Legal Services Facility (LSF),Joaquine De Mello, wakati wa Hafla ya miaka mitano ya shirika
hilo na kukabidhi fedha kwa mashirika mapya ya wanaufaika.
“Nimeweza
kuzunguka Magereza yote nchini na kujionea namna gani wafungwa walivyojazana
kwa wingi lakini robo tatu ya wafungwa waliopo humo ni mahabusu ambao awaja
hukumiwa” alisema Jaji Joaquine De Mello
Aliongeza kuwa
imefika wakati wa wasaidizi wa kisheria kuanza kuwasaidia watu kwa nagazi ya
vituo vya Polisi ambapo huko wanaweza kupata dhamana kabla ya kufika
magarezani.
Kwa upande
wake, Scholastica Julu, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo alisema kuwa
shirika hilo limeweza kutoa fedha zaidi ya Bilioni ishirini kwa mashirika
mbalimbali nab ado litaendelea kutoa hili kuweza kusaidia wasaidzi wa kisheria
na Mashirika yanayowasimamia .
Alisema kuwa
wameweza kupokea changamoto ya usafiri kwenye baadhi ya mikoa na kama shirika
wanalifanyia kazi hilo swala hili waweze kutatua tatizo hilo kwa wasaidizi
wanaofanya kazi hiyo kwa mazingira hayo magumu.
0 comments:
Post a Comment