Shirikisho
la Mpira wa Miguu Nigeria (NFA), limesogeza mbele kwa siku moja mchezo
kati ya timu ya taifa ya Nigeria ‘The Super Eagles’ na Tanzania ‘Taifa
Stars’ ambako sasa utafanyika Septemba 3, 2016 badala ya Septemba 2,
2016 iliyotangazwa awali.
Na
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kesho anatarajiwa
kutangaza kikosi ambacho atakiandaa maalumu kwa mchezo huo. Mkwasa
amesema kwamba anatarajia kuita wachezaji 20 ambao atasafiri nao kwenda
Nigeria kwa ajili ya mchezo huo.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hii BOFYA HAPA
IVORY COAST YAWASILI DAR, MECHI IJUMAA
Timu
ya Taifa ya Mpira wa Miguu Ufukweni ya Ivory Coast, imeingia Dar es
Salaam, Tanzania leo saa 8.00 usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la
Ethiopia ikitokea jijini Abidjan.
Timu
hiyo imekuja Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kuwania
nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu wa
ufukweni ambako itacheza na wenyeji Tanzania Ijumaa wiki hii kwenye
uwanja maalumu ulioandaliwa kwa ajili ya mchezo huo.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hii BOFYA HAPA
TFF YAIANDALIA SERENGETI BOYS KAMBI TULIVU
Baada
ya kutekeleza ahadi ya mwanzo ya kuipeleka Madagascar kwa ajili ya
kambi ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’, Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepanga kutekeleza ahadi yake
nyingine kwa kuipeleka timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa
chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kwenye kambi tulivu, ikiwezekana nje
ya nchi.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hii BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment