Nafasi Ya Matangazo

August 20, 2016

Naibu Waziri wa Wizara ya fedha na mipango Dkt Ashatu Kijaji, akikata utepe kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya Posta, Mjini Moshi lililopo katika Jengo la NSSF PLAZA nyuma yake Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Prof Lettice Rutashobya na wafanyakazi wa TPB wakishuhudia tukio hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya fedha na mipango Dkt Ashatu Kijaji kushoto, akikabidhiwa kadi ya Benki na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Prof Lettice Rutashobya (Kulia) baada ya kufungua akaunti katika tawi jipya la Benki ya Posta lililopo katika jingo la NSSF PLAZA.
Burudani ya Ngoma
Meza Kuu wakifurahia wakati wa Burudani ya Ngoma ikitumbuiza 
Naibu Waziri wa Wizara ya fedha na mipango Dkt Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Benki ya Posta baada ya Ufunguzi wa tawi la benki hiyo Mjini Moshi katika jingo la NSSF PLAZA, Kulia kwa Mgeni Rasmi ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Ritha Riwa.
***************
Benki ya Posta Tanzania (TPB) inayo furaha kubwa kuzindua rasmi tawi lake jipya hapa mkoani Kilimanjaro. Hili ni tawi ambalo tumelihamisha kutoka jengo la Horombo Lodge mtaa wa Old Moshi, kuja hapa kwenye jengo la NSSF Plaza.

Nia ya kuhamisha tawi letu kuja kwenye jengo hili ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi, na pia kutuwezesha kutoa huduma zetu kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi.  Tunawaahidi wakazi wa mkoa huu kuwa wataendela kufaidika na huduma zetu bora na zenye gharama nafuu kabisa katika mazingira haya yaliyoboreshwa. Pia watafaidika na mikopo ya aina mbalimbali tunayoitoa, inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa,mikopo ya  wafanyakazi na hata wastaafu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa tawi hili, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Sabasaba Moshingi alisema kuwa anaamini kwamba tawi hili jipya litaweza kuongeza idadi ya wateja kwenye banki yake. Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani benki yangu ianatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii. Benki ya Posta inapenda kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla kwa kutuamini na kuendelea kutumia huduma zetu. Tunaahidi hatutawaangusha, na tutaendelea kuboresha huduma zetu zenye gharama nafuu, alisema Moshingi.

Moshingi aliendelea kwa kusema kuwa TPB inaendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi, mwanzoni mwa mwaka huu benki ilifungua tawi lake jipya la Songea, Mkoani Ruvuma, pamoja na tawi la Babati Mkoani Manyara. 

Matawi hayo mawili yamejengwa kwenye viwanja vinavyomilikiwa na TPB. Pia Benki ipo kwenye mchakato wa hivi karibuni kufungua matawi mapya huko Same, Tarime mkoani Mara, Chato Mkoani Mwanza, Kondoa Mkoani Dodoma, na Tukuyu Mkoani Mbeya. 

Benki ilihamishia Makao yake Makuu kutoka jengo la Extelecoms lililopo mtaa wa Samora na kuhamia kwenye Jengo la Millenium Towers, Kijitonyama. Pia, benki hivi karibuni itahamisha matawi yake yaliyoko Kahama na Tanga kwenda kwenye majengo mapya na ya kisasa. Hizi zote ni jitihada za benki za kuongeza ufanisi na pia kutoa huduma zake kwenye mandhari bora naya kisasa zaidi.

Naye mgeni Rasmi kwenye uzinduzi huo, Naibu Waziri Mkuu wizara ya  Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji aliisifu benki ya Posta kwa jitihada zake za kupeleka huduma karibuu zaidi na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mawakala, na pia kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu ambazo kila Mtanzania anaweza kuzimudu. 

Mimi binafsi pamoja na Serikali yetu tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba sekta ya mabenki nchini inatoa msukumo unaotakiwa katika shughuli za kiuchumi nchini, na hasa katika kuwawezesha wazalishaji kuboresha ufanisi na tija, mambo ambayo ni msingi wa ukuaji wa haraka wa uchumi.  

Serikali imekuwa pia ikitoa msukumo kwa mabenki kupanua wigo wa shughuli za kibenki kwa kupeleka huduma hizo vijijini, kuweka riba na masharti nafuu kwa mikopo inayotolewa kwa wazalishaji mali ili mchango wa sekta hii katika pato ghafi la Taifa uweze kukua. 

Vile vile Serikali imekuwa ikitoa msukumo kwa sekta ya mabenki pamoja na sekta zingine juu ya umuhimu wa kutumia teknolojia ya kisasa katika uzalishaji na utoaji wa huduma kwa kuamini kwamba teknolojia bora huwezesha katika kuboresha ufanisi, kupunguza gharama na kupanua wigo wa soko, alisema Mhe.Kijaji.

Naye Meneja wa Benki ya Posta tawi la Moshi Web Msuya akizungumza kwenye uzinduzi huo alisema napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wajasiriamali, wanavikundi, wastaafu, wafanyakazi na hata wanafunzi wa hapa moshi, kuja kufungua akaunti kwenye tawi letu hili jipya. Tunazo akaunti maalum kwa ajili yenu wote, na tutawapa huduma bora na ya haraka. 

Pia napenda kuzikaribisha taasisi mbalimbali zilizopo hapa mkoani, vikiwemo vyuo,mashirika na hata mashule, kuja kufungua akaunti za taasisi zenu kwetu, nasi tunaahidi tuwapeni huduma bora na za kisasa. Ninaamini mtanufaika sana na huduma zetu zenye gharama nafuu. 
Posted by MROKI On Saturday, August 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo