Benki ya NMB kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Women's World
Banking leo wamezindua mpango wa kuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa
kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi
ya baadae. Mpango huo umepewa jina la WAJIBU mahususi kwaajili ya akaunti za
akiba za watoto navijana.
WAJIBU yenye maana ‘Wajibika’
inajumuisha aina tatu za akaunti za akiba: NMB Mtoto Akaunti, NMB Chipukizi Akaunti na
NMB Mwanachuo Akaunti zilizotengenezwa kwaajili ya vijana katika kila
hatua ya maisha yao huku lengo likiwa kuwasaidia wazazi na vijana kujiwekea
akiba na kupanga matumizi wao wenyewe au kwa msaada wa wazazi ili kutimiza azma
yao.
NMB Chipukizi Akauntini akaunti ya
kipekee na maalumu kama akaunti ya kwanza ya aina yake kutambulishwa nchini,
akaunti hii ni maalumu kwa vijana wenye umri kati ya miaka 13 mpaka miaka 17 na
wanamiliki akaunti hiyo kwa majina yao. Akaunti hizi zinaunganishwa na msemo
kuwa JIfunze,
Jipange – WAJIBIKA!Mpango huo mahususi kwajili ya kuwawezesha watoto na
wazazi kujua masuala ya kifedha na jinsi ya kutumia taasisi za kifedha
kujiwekea akiba kwa maendeleo.
Akiongea kwenye uzinduzi wa WAJIBU, Mkurengezi
Msaidizi wa Udhibiti na Ubora wa Shule Dk. Edicome Cornel Shirima kutokea Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
– alisema “Walaji wenye uwezo, wanaojiamini na
walioshirikishwa wanaofanya maamuzi sahihi ya kifedha situ wataboresha maisha
yao bali jamii kwa ujumla. Ninafarijika sana leo kuzindua mpango huu wa WAJIBU
kwani nina Imani kuwa utasaidia kuwapatia watoto na wazazi stadi muhimu
zitakazowawezesha kupanga maisha yao ya baadae.”
Hii ndiyo maana serikali imedhamiria kwa dhati kabisa kuboresha na
kuendeleza elimu ya fedha katika ngazi zote za watanzania – Hususani wanajamii
yote ya Tanzania, aliongeza Dk. Shirima
Jifunze, Jipange - WAJIBIKA! Inajumuishavipindi vitatu kwaajili ya shule za sekondari na msingi –Kipindi cha kwanza kitazingatia mafunzo ya elimu ya masuala ya fedha na taasisi za kifedha itakayowaunganisha wanafunzi na wazazi wao, na kufuatiwa na vipindi viwili maalumu kwa watoto wenyewe. Katika mafunzo hayo, washiriki watajifunza umuhimu wa kuweka akiba benki, jinsi akaunti ya benki inavyoweza wasaidia kupanga matumizi ya fedha zao, kutengeneza malengo ya kuweka akiba na kuweka mkakati wa kuweka akiba, kufungua akaunti ya WAJIBU na kuanza kuitumia.
“Tumefarijika sana kushirikiana na mashule ili kukamilisha mpango huu, utayari wao katika kusaidia wanafunzi kupata elimu hii itasaidia sana kuwajengea wanafunzi maisha mazuri ya baadae” alisema Bi Ineke, mkurugenzi mtendaji wa NMB Benki.
0 comments:
Post a Comment