Baadhi
ya wafanyakazi wa TBL Group wakionyesha medali zao muda mfupi baada ya
kumalizika kwa matembezi
Baadhi
ya wafanyakazi wa TBL Group na familia zao katika picha ya pamoja muda mfupi
baada ya kumalizika kwa matembezi yaliyotayarishwa na taasisi ya Ocean Church.
WAFANYAKAZI wa kampuni ya TBL Group wamepongeza
hatua ya kampuni kutekeleza mpango wa Afya kwanza ambao unawawezesha kujua hali
ya afya zao wakiwa kazini,kujengewa mazingira ya kufanya mazoezi na familia zao
na kupatiwa ushauri wa jinsi gani ya kukabiliana na changamoto za
magonjwa ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi nchini.
Wakiongea baada ya kumaliza kushiriki mbio za
kilometa 5 zilizotayarishwa na taasisi ya Ocean Church na kufanyika
jijini Dar es Salaam baadhi yao walisema kuwa utaratibu huu ni wa muhimu
wa kuwawezesha kushiriki katika mazoezi kwa ajili ya kuweka afya zao na familia
zao vizuri.
Akiongea kwa niaba ya wafanyakazi wenzake
baada ya kumalizika zoezi hilo la utekelezaji wa progamu ya Afya Kwanza Sam
Mhagama kutoka TBL Ilala alisema kuwa mpango huu ni mzuri kwa kuwa unawawezesha
wafanyakazi kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara,kupata
ushauri wa kitaalamu na kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Kwa upande wake Seleman Mbena alisema kuwa
utaratibu wa kusogeza huduma za afya sehemu za kazi na kufanya mazoezi ni
mzuri kwa kuwa unawawezesha wafanyakazi kupata elimu ya kujikinga na maradhi
mbalimbali na wale wanaosumbuliwa na maradhi wanapata elimu ya jinsi ya
kukabiliana nayo pia wanapata elimu ya lishe bora na jinsi ya kukabiliana na
changamoto ya magonjwa hasa yanayosababishwa na maisha ya kisasa wanayoishi
wafanyakazi wengi.
Mratibu wa Programu ya Afya Bora wa kampuni ya
TBL Group,Julieth Mgani alisema Japo suala la afya limekuwa halipewi kipaumbele
na waajiri wengi nchini lakini ni suala muhimu la kuzingatiwa na waajiri
wengi ili kuleta tija na ufanisi, kwa kuwa wafanyakazi wenye afya bora
wanashiriki vizuri katika shughuli za uzalishaji
Alisema Afya Bora kwa wafanyakazi haina
maana wafanyakazi kulipiwa gharama za matibabu mahospitalini na waajiri
wao bali inahusisha mambo mengi kuhusiana na afya zao na afya za familia
zao.
Mgani alisema Alisema katika sehemu za
kazi suala la Afya linapaswa kuzingatiwa wakati wote sio kulipa kipaumbele mara
chache wakati wa kuadhimisha siku ya Afya au ya ugonjwa fulani kama ambavyo
imekuwa mazoea kufanyika na siku hiyo ikipita hakuna kinachoendelea.
0 comments:
Post a Comment