Jengo hili limejengwa lilipokuwa Jengo la zamani la Salamanda katika Makutano ya mtaa wa Samora na Azikiwe Dar es Salaam limeshika moto katika gorofa yake ya pili na kuharibu baadhi ya mali. Chanzo cha moto huo katika jengo hilo linalomilikiwa na Mfanya Biashara maarufu Yusuf Manji kupitia Kampuni yake ya Quality Boulevard bado hakijabainika.
Moto
umeteketeza baadhi ya mashine za viyoyozi vilivyokuwa vimehifadhiwa katika
ghorofa ya pili katika jengo jipya la Salamanda mali ya Quality Boulevard ya
jijini Dar es Salaam lililopo katika makutano ya mtaa wa Samora na Mkwepu. Moto
huo ulianza jana jioni na kuwaka kwa zaidi ya nusu saa ndipo kikosi cha Jeshi
la Zimamoto kilipowasili na kuzima moto huo.
Moto huo ukiwaka kwa ndani kama unavyoonekana na kuteketeza viyoyozi hivyo vilivyohifadhiwa tayari kwa kufungwa katika jengo hilo.
Wafanyakazi waliokuwa ndani ya jengo hilo wakitoka.
Gari la zima moto STL 4920 likifika eneo la tukio.
Wanancghi wakiwa pembezoni mwa mtaa wa Samora wakiangalia moto huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Polisi walikuwepo kulinda usalama
Wananchi walikaa katika vikundi kujadili moto huo.
Magari matatu ya Kikosi cha Jeshi la Zimamoto STL 4920, STL 4927 na STK 1066 yalifika na kuuzioma moto huo ambao tayari ulisha teketeza majokofu hayo.
Wananchi wakishangaa
Kibao cha Mkandarasi wa Jengo hilo AQE Associates LTD
0 comments:
Post a Comment