Uongozi na wanachama wa Chama cha wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Emilio Senga kilichotokea Julai 27, huko New Dehli nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Senga alikwenda nchini India kwaajili ya matibabu ya Moyo Julai 12, mwaka huu ambapo Julai 19 alifanyiwa upasuaji wa mmoja ya mishipa moyo na kumalizika salama na Julai 27 kuruhusiwa kutoka Hospitalini lakini hali yake ilibadilika na kurwejeshwa tena Hospitalini na ilipofika saa 1:15 usiku alifariki.
Kifo cha Semnga si tu pigo kwa familia yake lakini ni pigo kubwa kwa wanahabari na wapigapicha wote nchini Tanzania hasa kutokana na uchapakazi shupavu uliosheheni weledi .
PPAT inaungana na familia yake na wote waliofikwa na msiba huu mzito katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo .
Aidha taarifa iliyotolewa jana
na Kampuni ya Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, ilisema
kuwa taarifa rasmi ya lini mwili wa marehemu utarejeshwa nchini uitatolewa
kesho ikiwa ni pamoja na mipango mingine ya kuaga mwili wa marehemu na
kuusafirisha hadi Kijijini kwao Mkoani Mwanza kwa mazishi.
Aidha Chama cha Demokrasia na
Maendeo Chadema kimetuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mpigapicha huyo
na kumuelezea marehemu kama Shujaa wa Demokrasia na Haki.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETYWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Marehemu Joseph Senga
enzi za uhai wake. Kama taasisi na kisha mtu mmoja mmoja kuanzia kwa
wanachama na viongozi wa chama kwa hatua ya sasa tumejikuta tumeishiwa
maneno ya kusema kuhusu kifo cha mwandishi huyu mwandamizi, lakini
katikati ya mshtuko na majonzi tuliyonayo, tunaweza kusema kuwa kifo cha
Senga, hasa siku kiliyotokea, kimedhihirisha jambo moja kubwa kuwa
alikuwa SHUJAA WA DEMOKRASIA NA HAKI. Kifo cha Senga kimetokea siku
ambayo kulikuwa na matukio makubwa mawili kuhusu demokrasia na haki
nchini. Kwanza, wakati Senga anafariki usiku wa Jumatano, Julai 27,
mchana wa siku hiyo hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, ilikuwa imetoa
hukumu ya kifungo cha miaka 15 jela askari anayefahamika kwa jina la
Pacificius Simon kwa hatia ya kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, mkoani Iringa. Matukio
hayo matatu; kuuwawa kwa Mwangosi, hukumu ya aliyemuua na kifo cha
Senga, yana uhusiano mkubwa wa karibu huku Senga akiwa katikati yake,
kwamba; Picha zote ambazo hadi leo zinaweza kupatikana dunia nzima
kupitia mtandao wa intaneti zikionesha mauaji ya kikatili aliyofanyiwa
Mwangosi, kuanzia ile ambayo inaonesha kundi la askari polisi likiwa
limemzunguka Mwangosi huku mmoja wao akiwa amemlenga kwa bunduki ya
kulipulia mabomu ya machozi, hadi zile ambazo zinaonesha mwili wa
mwandishi Mwangosi ukiwa umefumuliwa na kutawanywa vibaya baada ya
kulipuliwa, huku nyingine ikimuonesha mmoja wa askari akiugulia maumivu
ya ‘bomu’ lililomuua Mwangosi, zilipigwa na Shujaa Senga. Kwa watu
waliokuwepo siku ya tukio hilo baya kuwahi kuikumba tasnia ya habari
nchini, watakumbuka kuwa Senga alipiga picha zile akiwa katikati ya
mirindimo na moshi wa mabomu, ngurumo za risasi za moto na kundi la
askari wengi ambao walikuwa wanazidi hata idadi ya wanachama na viongozi
wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika kwa amani kwenye ofisi yao kijijini
Nyololo kabla hawajavurugwa na Jeshi la Polisi likiongozwa na RPC
Michael Kamhanda. Picha zile ambazo ziliiambia dunia nzima ukweli wa
tukio hilo, ziliokoa watu wengi na bila shaka zilisaidia kutotokea kwa
jambo kubwa ambalo watawala walishaanza kuonesha nia ya kulitekeleza,
kupitia maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, makao makuu na mkoani
Iringa, ambao walitaka kuonesha kuwa CHADEMA ‘walijilipua’, ambapo maana
yake ni kwamba wafuasi, wanachama na viongozi wa CHADEMA walikuwa na
milipuko au vitu vya namna hiyo. Pili; Senga amefariki siku ambayo
Watanzania bila kujali tofauti zao, wakiongozwa na CHADEMA walitangaza
Operesheni UKUTA ambayo moja ya malengo yake ni kupigania haki za
makundi mbalimbali ya Watanzania, wakiwemo waandishi wa habari dhidi ya
mifumo kandamizi inayolelewa na watawala kupandikiza mbegu za utawala wa
kidikteta nchini. Kwa muda mrefu, kupitia chombo chake alichokuwa
akikifanyia kazi hadi mauti yanamkuta, Free Media, CHADEMA kama
inavyofanya kazi na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali, ilikuwa
ikishirikiana na Senga kikazi, huku naye akifanya kazi yake kwa uwezo
mkuwa, akizingatia miiko na misingi ya taaluma ya uandishi wa habari,
kwa weledi mkubwa. Habari picha zake mbalimbali ambazo zimekuwa
zikidhihirisha ukongwe wake katika tasnia ya habari, zikiwemo za matukio
ya CHADEMA, zitakuwa historia itakayotunza jina lake miongoni mwa
waandishi mahiri nchini ambazo waandishi chipukizi watajifunza. Kwa
masikitiko makubwa, CHADEMA inatoa salaam za pole kwa familia ya
marehemu, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, wafanyakazi
wenzake, tasnia ya habari nchini na Watanzania wengi walioguswa na msiba
huo. Mwenyezi Mungu awatie moyo wa ujasiri kuyakabili majonzi mazito ya
kifo cha mpendwa Senga. Huyo ndiyo Joseph Senga. Shujaa wa demokrasia
na haki. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Imetolewa leo
Alhamis, Julai 28, 2016 na; Tumaini Makene Mkuu Idara ya Habari na
Mawasiliano CHADEMA
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
0 comments:
Post a Comment