Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na wafanya biashara wakubwa na wadogo na watoa huduma mbalimbali zikiwepo za usafiri wa bodaboda katika mkutano aliouitisha kwa lengo la kufahamiana na kusikiliza kero zao pamoja na kuwapa mwongozo wa kile serikali inachokitaka.
Meza kuu ikisikiliza maoni ya wafanya biashara hao.
Wafanyabiashara w mkoa wa Mbeya wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa MKOA wa Mbeya Amos Makalla amewahaidi kuwapa ushirikiano jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya ili waweze kufanya biashara katika mazingira mazuri kwa kushughulikia changamoto zinazowakabili huku akipenda watendaji wa serikali wanaondekeza rushwa na urasimu katika biashara na uwekezaji.
Hayo ameyasema leo katika kikao alichokiitisha yeye mwenyewe Mkuu wa Mkoa kwa kuzungumza na wafanyabiashara wenye viwanda, wafanyabiashara wakubwa na kati, wenye mahoteli, wasafirishaji, wasindikaji wa Mazao , wawakilishi wa masoko , bodaboda , daladala na bajaji ili kujitambulisha na kuwapa mwelekeo wa serikali pamoja na kusikiliza kero zao.
Aidha mkutano huo ulihusisha wawakilishi wa mabenki, mamlaka ya mapato,mamlaka ya udhibiti wa chakula, Tanesco, jeshi la polisi na wakuu wa idara mbali mbali za serikali.
Mkuu wa Mkoa amewaomba ushirikiano wafanyabiashara kwani serikali inategemea kodi hivyo ni jukumu la wafanyabiashara kulipa kodi na serikali itafanya kila linalowezekana kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ikiwemo kushughulika na watumishi wanaoendekeza rushwa na urasimu kwa wafanyabiashara.
Makalla amewahakikishia wananchi na wafanyabiashara kuwa tatizo la uhaba wa sukari karibia linaisha kwani kuanzia leo mkoa wa Mbeya utapokea sukari tani zaidi ya 1000 kutoka malawi na pia kiwanda cha Kilombero kimeanza uzalishaji na wiki hii Mkoa utapokea tani 500 kutoka kilombero.
Amewaagiza wafanyabiashara kutokaa na sukari Bali waiuze haraka iwafikie wananchi kwa haraka na kadri sukari itakavyozidi kupatikana na kusambazwa bei itapungua
0 comments:
Post a Comment