Nafasi Ya Matangazo

May 05, 2016


Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Gabriel Msovela akimpongeza Profesa Joseph Kahamba ambaye ni Kaimu Mratibu wa Kambi tiba ya vichwa vikubwa na migongo wazi inayoendelea kuzunguka nchi nzima

MEZA KUU: Kutopka kushoto ni Shannon Kiwamba, Meneja Miradi wa GSM Foundation, Khalfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano GSM, Profesa Joseph Kahamba, Kaimu Mratibu wa Kambi tiba ya vichwa vikubwa kutoka MOI, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Gabriel Msovela na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bw Nuru Hussein Mpuya
Picha ya pamoja.
******************
Na Mwandishi Wetu
kambi tiba ya vichwa vikubwa na mgongowazi inayofadhiliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation imemaliza kazi leo jijiji Shinyanga huku changamoto nyingi za huduma za kiafya zikiainishwa na viongozi wa mkoa huo, ambapo pamoja na mambo mengine wameiomba Taasisi hiyo kuitupia jicho sekta ya Afya mkoani humo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Akiongea na watumishi wa Afya walioshiriki zoezi hilo kutoka hospitalini hapo, na wale waliosafoiri kutoka Taasisi ya Upasuaji na Mifupa ya Muhimbili, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Albert Gabriel Msovela ameishukuru taasisi ya GSM kwa uamuzi wake unaoonekana kuwa ni wa busara sana na wa kizalendo wa kuamia kusaidia sekta ya Afya hasa kwa watoto.


Bw Msovela amekiri kuwepo kwa imani za kishirikina katika kanda ya Ziwa ambayo hupelekea wazazi wengi huamua kuwatibu watoto wao kwa kupitia imani za kishirikina na kuziacha tiba za kisayansi ambazo ndizo haswa zenye mashiko hasa katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia.



Katibu huyo Tawala pia alieleza changamoto za uhaba wa majengo katika hospitali ya mkoa ambapo wameanza ujenzi wa majengo mapya ya Hospitali itakayokidhi mahitaji ya wakazi wa mkoa wake, na kuiomba taasisi ya GSM iwapo itakuwa ndani ya uwezo wao, washiriki katika ujenzi wa hospitali hiyo kama wadau.



Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya GSM, Afisa Mawasiliano wa Taasisi hiyo Halfan Kiwamba ameahidi kulifikisha ombi la viongozi wa mkoa huo katika ngazi za juu ambapo bila shaka litafanyiwa kazi.



Kambi tiba ya vichwa vikubwa na Mgongo wazi kuanzia Ijumaa itakuwa ikitoa huduma mkoani Singida ambapo huduma za upasuaji zitatolewa kwa watoto chini ya miaka mitano kwa siku tatu mfululizo.



Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Nuru Hussein Mpuya, ameishukuru sana Taasisi ya GSM kwa kuonesha njia kwa wadau wengine katika hali ya kuhamasisha kumaliza changamoto za kiafya bila kuangalia bajeti za kiserikali.



Dk Mpuya amekitaja kitendo cha kufadhili kambio tiba na kufuatilia utendaji wake kuwa ni kitendo cha kizalendo kinachostahili kuigwa na makampuni mengine.
Posted by MROKI On Thursday, May 05, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo