Meneja Mauzo na Usambazaji wa Dar Brew, Fred Kazindogo (kulia) akizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa chupa mpya yenye
ujazo wa 750Mls ambayo itakuwa ikiuzwa kwa bei ya sh 1,000. Katikati ni Meneja masoko wa DarBrew Oscar Shelukindo na kushoto ni mwakilishi wa mauzo
Agripina Kusa
Meneja masoko wa DarBrew Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa chupa mpya yenye
ujazo wa 750Mls ambayo itakuwa ikiuzwa kwa bei ya sh 1,000, Kulia ni Meneja
mauzo na usambazaji wa Dar Brew Fred Kazindogo.
Meneja masoko wa DarBrew Oscar Shelukindo (kulia) akizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa chupa mpya yenye
ujazo wa 750Mls ambayo itakuwa ikiuzwa kwa bei ya sh 1,000, kushoto ni mwakilishi wa mauzo
Agripina Kusa
Meneja masoko wa DarBrew
Oscar Shelukindo katikati mwenye miwani akizungumza na waandishi wa Habari
jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa chupa mpya yenye ujazo wa 750Mls ambayo
itakuwa ikiuzwa kwa bei ya shilingi elfu moja,Kulia ni Meneja mauzo na
usambazaji wa Dar Brew Fred Kazindogo na kushoto ni mwakilishi wa mauzo
Agripina Kusa na Neema Mvungi mwenye fulana nyeupe.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Dar Brew jana ilizindua chupa mpya ya bia ya asili ya
Chibuku Super yenye ujazo wa milimita 750, ambayo mtumiaji halazimiki kurudisha
chupa pale anapoitumia.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana,
Meneja Masoko wa Dar Brew, Oscar Shelukindo alisema, bia hiyo iliyopo katika
chupa nzuri ya plastiki inayovutia, itauzwa kwa bei ya Sh 1,000 tu kwa kila
chupa.
“Leo (jana) ni siku ya furaha kubwa sana kwetu Dar Brew na kwa
watumiaji wote wa bia, kwani tumefanikiwa kuzindua chupa hii itakayouzwa kwa
bei nzuri ya Sh 1,000 tu na kwa ujazo unaotosheleza.
“Bia hii imetengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu na kwa kutumia
mitambo ya kisasa kabisa, hivyo tunawahakikishia watumiaji ubora wa hali ya
juu,” alisema.
Shelukindo alisema, bia hiyo imetengenezwa kwa kutumia malighafi za
hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mtama ulio bora, hivyo kuna kila sababu
kwa Watanzania kujivunia kilicho chao na kukumbuka asili yao, kwani hii ni bia
yao ya asili.
“Chibuku Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachokufanya uitumie kwa
muda mrefu ukiwa na marafiki, lakini inakupa lishe nzuri kutokana na
virutubisho vinavyopatikana katika nafaka zilizotumika kutengeneza bia hii.”
Naye Meneja Mauzo na Usambazaji wa Dar Brew, Fred Kazindogo alisema,
bia hiyo itaanza kupatikana nchi nzima katika baa, maduka makubwa (Super
Markets), katika maduka ya jumla na rejareja na sehemu zinazouzwa vileo kuanzia
leo.
“Tunatarajia wateja na wapenzi wa bia wataifurahia chupa hii mpya na
kwa wauzaji wa jumla, tunaamini watahamasika kuuza Chibuku Super kwani ina
faida nzuri na haina usumbufu wa kununua chupa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment