Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki
akikabidhi madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga
Theresia Msuya yaliotolewa na Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo
Kanda ya Kaskazini George Lugata.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck
Sadiki(Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Mwanga Theresia Msuya(katikati) Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini
George Lugata
**************
KAMPUNI ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa
madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa shule nane za msingi
katika manispaa ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni mchango wa kampuni
hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule
za msingi nchini.
Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano
iliyofanyika katika shule ya msingi Reli Juu katika manispaa ya Mwanga,
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata amesema mchango huo ni
sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada
mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali
zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa
jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika
kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo
madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Lugata.
Lugata amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi
msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga,
Mbeya Iringa na Morogoro na kuongeza
kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini
siku za zijazo.
Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro mheshimiwa Meck Sadiki ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha
mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Kilimanjaro na kutoa wito kwa
wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.
“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa
kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za
kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za
msingi za mkoa wetu wa Kilimanjaro. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati
400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo
kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Sadiki
Madawati hayo yametolewa kwa shule za
msingi nane kama ifuatavo,
Mramba,Kawawa, Mwanga, Naweru,Kiboriloni, Lawate na Reli Juu.
0 comments:
Post a Comment