Muonekano wa barabara ya Nyakahura-Rusumo
inayounganisha Tanzania na Rwanda kupitia Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Mtaalam kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), wa pili kulia akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia), alipotembelea ofisi hizo
katika Kituo cha pamoja cha forodha (One
Stop Border Post) upande wa Tanzania kilichopo Rusumo wilayani Ngara, wa
kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa ufafanuzi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (mwenye kofia) wakati akikagua
maandalizi ya ufunguzi wa Daraja la Rusumo na Vituo vya pamoja vya forodha (One Stop Border Post) wilayani Ngara.
Muonekano wa Daraja la Rusumo
linalounganisha Tanzania na Rwanda, kushoto ni daraja la zamani lenye rangi ya
njano na kulia ni daraja jipya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) na Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale wakati akikagua
Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Meneja wa Kituo cha pamoja cha
forodha(One Stop Border Post), katika
mpaka wa Tanzania na Rwanda upande wa Rwanda Bw. Moses Kalisa akitoa maelezo
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na ujumbe
wake walipotembelea kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment