HAWA NDO KUMI BORA
Majina kumi ya mwanzo wanao wania kinyang`anyiro cha kumsaka kijana mwenye wazo zuri la kibiashara na atimae mchanganuo wa biashara Heroes Of Tomorrow Business Competition yametajwa jana na maneja wa shindano hilo bw. Erick Mchome, kwenye barua ya mwaandishi iliyotolewa na meneja wa Staitoil nchini Bw. Qystein Michelsen.
Heroes of tomorrow ama Mashujaa wa kesho ni shindano linaloendeshwa na kampuni ya mafuta na gesi kutoka Norway hapa nchini kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi ya Tanzania kwa kutafuta vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 25 ambao watakuwa na mawazo mazuri ya biashara ili kuwasaidia katika ndoto zao hizo kwa kufanya kuwa kweli.
“Shindono linalenga vijana kutoa mawazo yao ya kibiashara amabayo baadae yatafanywa kuwa biashara” alisema meneja wa shindano hilo Bw. Mchome Shindano hilo limeanza na vijana wa Lindi na Mtwara ambapo vijana 400 walijitokeza kushiriki wakilenga maswala ya kilimo, ufugaji, IT, viwanda vidogodogo na maswala mengine yanayohusiana na biashara ambapo baadhi walijikusanya kama kikundi na wengine mmoja mmoja.
40 bora walichaguliwa kushiriki katika mafunzo ya ujasilia mali yaliyo lenga kukuza na kuendeleza biashara ili ziwe na mafanikio ambapo katika hilo kumi
bora walichanguliwa.
Walio chagulia kumi bora ni Razaki Kaondo, Nyenje Chikambo, Edward Timamu, Saleh Rashid Kisunga, Azizi Doa, Sifael Nkiliye, Said Selemani, Yunus Mtopa, Yahay Omari, Kastus Kambona na Abdalah Selega. Hata hivyo mchakato bado unaendelea kwani kumi.
hawa watachuana vikali kwa kuleta michanganua yao ya biashara ambayo itafanyiwa tasmini na baraza la Jury ili kuwapata tano bora na atimae mshindi.
“Tano bora watatetea michanganuo yao ya biashara mbele ya baraza la Jury” alisema Bw.Mchome ikiwa ni sehemu ya kumtafuta mshindi wa shindano hilo.
Mshindi atapatikana tarehe 15 April jijini Dar es salaam, atazawadiwa dola za kimarekani 5000 wanne walio ingia tano bora kila mmoja wao atajipatia dola 1500 na waliofanikiwa kuingia kumi bora kila mmoja wao atapata dola 1000
0 comments:
Post a Comment