Dk Ayoub Rioba, Mkurugenzi Mkuu mpya wa TBC
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa
mujibu wa mamlaka aliyonayo.
KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa
Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba
28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka
ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.
Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt.
Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub
Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement
Mshana ambaye amestaafu.
TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa
Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania
(RAHCO).
Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi
Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja
0 comments:
Post a Comment