Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo( kulia) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini
Tanzania, Thami Mseleku( katikati) pamoja na Patiwe Makoena Afisa
anayeshughulikia masuala ya siasa katika ubalozi wa Afrika Kusini.Wakati wa
Kikao na Waziri wa Nishati nishati na madini, pamoja na watendaji wa taasisi
zilizochini ya wizara hiyo hawapo pichani.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo( kushoto) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami
Mseleku.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo( kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Afrika Kusini
nchini Tanzania, Thami Mseleku( kulia ) pamoja na watendaji wa Taasisi
zilizochini ya Wizara ya Nishati wakati wa kikao na ujumbe kutoka nchini Afrika
Kusini waliotaka kufahamu zaidi fursa za uwekezaji nchini Tanzania.
**********
WAZIRI wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa milango ya uwekezaji iko wazi kwa Mataifa
yote duniani yenye nia thabiti ya kufanya hivyo nchini Tanzania. Anaandika Zuwena Msuya wa Wizara ya Nishati na Madini. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Profesa Muhongo alisema hayo
jijini Dar Es Salaam wakati wa kikao chake na Balozi wa Afrika Kusini hapa
nchini,Thami Mseleku, ambaye alifika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kufahamu
zaidi fursa za uwekezaji kwa ajili ya manufaa ya Kampuni za uwekezaji za Afrika
Kusini .
Katika kikao hicho, Profesa
Muhongo alimueleza Balozi Mseleku kuwa Tanzania ina fusra nyingi za uwekezaji
katika masuala ya Nishati na kutaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na makaa ya
mawe, Nishati jadidifu,Upepo,mawimbi ya bahari pamoja na umeme wa jua.
Aidha Profesa Muhongo alimueleza
Balozi Mseleku kuwa Kampuni za uwekezaji kutoka Afrika Kusini zimekuwa
zikifanya vizuri katika Sekta ya Madini hasa katika kulipa mirabaha na tozo
mbalimbali za zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.
Vilevile Waziri wa Nishati na
Madini alimsisitiza Balozi huyo wa Afrika Kusini kusini kuwekeza katika sekta
ya gesi ambayo tayari inapatikana hapa nchini ili kuzalisha umeme kwa kuwa
Tanzania inahitaji umeme mwingi, wa uhakika na wa kutosha.
Profesa Muhongo alieleza kuwa
Tanzania inatarajia kufikia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 utakaotokana
na uwepo wa nishati ya umeme ya kutosha nchini, pia tayari imesaini Mpango wa
Umoja wa Mataifa unaoelekeza kila mtu kupata huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030
unaofahamika kama " SE4ALL" Nishati Endelevu kwa wote.
Kwa upande wake Balozi Afrika
Kusini hapa nchini, Thami Mseleku,alisema kuwa inchi yake ipo tayari kuwekeza
katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati ya gesi, mafuta na makaa ya mawe na
kwamba nchi hiyo inauzoefu zaidi katika uwekezaji wa nishati ya makaa ya mawe.
Balozi huyo wa Afrika Kusini katika Mkutano huo aliambatana na Afisa
anayeshughulikia masuala ya siasa, Patiwe Makoena.
0 comments:
Post a Comment