Kaimu Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro
Shirika la Majisafi na
Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwako na ongezeko la Maji katika
maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, pamoja na maeneo ya miji ya Kibaha
na Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini kuanza kufanya
majaribio ya uzalishaji wa Maji .
Akiongea na waandishi wa
habari Kaimu Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro , amesema kuwa kutokana
na ongezeko hilo la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na pia
kumekuwepo na ongezeko la uvujaji wa Maji katika maeneo mengi ya jiji la Dar es
salaam, hasa katika maeneo ambayo yalikuwa na miundombinu ya Maji lakini
hayakuwa na huduma ya Maji na baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji
kwa msukumo mdogo (Low pressure)
“Kufuatia ongezeko hili la Maji watu wengi wameanza kupata huduma
ya Majisafi, na uvujaji wa Maji umeongezeka katika maeneo ambayo aidha yalikuwa
na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji au maeneo ambayo
yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo mdogo”
Alisema Bi. Lyaro
Aidha, ametoa wito kwa wateja
na wananchi wote kutoa taarifa za uvujaji huo wa Maji pindi wanapobaini kuwapo
na uvujaji wa Maji katika makazi yao na maeneo mbalimbali ya jiji kupitia kituo
cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 022194800 au 0800110064 (Bure).
“Namba hizi ziko wazi saa 24
kwa siku na mteja hatakatwa gharama yoyote akipiga simu hizi. Hivyo tunaomba
wateja wetu waisaidie Dawasco kupunguza upotevu wa maji kwa kutupa taarifa za
mivujo na kupasuka kwa mabomba” alisema bi Lyaro.
Kutokana na ongezeko hilo la
Maji maeneo yaliyoanza kupata Maji baada ya majaribio ya mtambo huo kuwa ni
Tandale,Manzese makunimula,Mwananyamala,Kinondoni mkwajuni, baadhi ya maeneo ya
vingunguti,changombe,ubungo-mabibo na city centre.
Pia, DAWASCO imetumia nafasi
hiyo kuwakumbusha wateja wote kulipia huduma ya Maji kwa wakati kwani watu
wengi kwa sasa wameanza kupata huduma ya Majisafi na salama kutokana na
kuongezeka kwa uzalishaji wa Maji katika mtambo wa Maji wa Ruvu chini, hivyo
hawana budi kuyalipia ili kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma ya Maji.
Kuongezeka kwa huduma ya Maji
katika jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kumetokana na kukamilika upanuzi wa mtambo wa
Ruvu chini ulioanza mwaka 2011 hivyo kuongezeka kiasi cha uzalishaji wa Maji
kutoka wastani wa lita milioni 182 hadi lita 270 kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment