Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku (kushoto)akisoma taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA
Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM mkoa wakisikiliza wakati Kaimu Katibu wa Mkoa Ndugu Mary Maziku akiwakilisha taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Singida mara baada ya kupokea taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi jengo la CCM mkoa wa Singida ikiwa sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la mtama la mkulima wa kujitegemea Elisha Mdaa (kushoto) katika Kata ya Mtamaa, Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani Singida kesho. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuhimiza kila mwananchi kuchapa kazi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Unyianga, Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani Singida kesho kutwa.
Komredi Kinana akihutubia baada ya kushiriki ujenzi wa majengo ya shule ya Unyianga ambapo alihimiza wananchi kuwa na moyo wa kujitolea katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya kijamii pamoja na kujenga tabia ya kuchapa kazi.
Mkulima wa mfano wa shamba la mtama lililotembelewa na Komredi Kinana, Elisha Mbaa akielezea jinsi anavyotumia jembe la kukokotwa na ng'ombe katika kilimo hicho, ambapo katika heka moja na nusu huvuna magunia 15 ya mtama na fedha zinazopatikana kwa kuuza mtama huo zinasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji mengine.
Katibu wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Singida, akisoma risala ya pamoja ya wajasiriamali wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana mjini Singida leo. Komredi Kinana alitumia wasaa huo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wajasiriamali.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Mwajuma wakati wa mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa kesho kutwa mjini Singida.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Hawa Mtipa wakati wa mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa kesho kutwa mjini Singida.
Komredi Kinana akizungumza na wajasiriamali mjini Singida leo
Ofisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Erick Sinkwembe akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa Wajasiriamali wa manispaa hiyo, kuhusu uendeshaji wa mafunzo kwa waendesha Bodaboda pamoja na utekelezaji wa sheria mbalimbali za kodi ambazo mara nyingine si rafiki kwa wajasiriamali. Mkutano huo ulifanyika katika Jengo la Ofisi ya CCM ya Mkoa huo.
0 comments:
Post a Comment