Fastjet
Tanzania imeongeza ndege nyingine aina ya Airbus A319 kwenye idadi ya ndege zake nne na hivyo kuliweka shirika hilo la ndege la
gharama nafuu kuendelea na mipango yake ya kupanuka.
“Ndege
za fastjet kwa hivi sasa ni nne na zote zinatumika na ongezeko la ndege ya tano ni jibu kwenye mikakati yetu ya kupanuka pamoja na hitaji la kuongeza uwezo
wa kubeba kwenye safari zetu za ndani na za kimataifa”, alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.
Ndege
hiyo ya nyongeza inafanya jumla ya
nafasi inayokuwepo kwa siku kwenye safari kwa ajili ya wateja kufikia 1,000.
Fastjet
ilianza safari zake nchini mwaka 2012na hivi sasa inajiendesha kwa kutumia
ndege tano aina ya A319 kwenye mtandao
wake wa safari ambao unahusisha Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro na
Zanzibar na kuifanya ijikite kuufanya usafiri wa anga ndani ya Tanzania watu
wote waumudu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hali
kadhalika ilianzisha safari za kimataifa
kwenda Entebbe nchini Uganda, Nairobi Kenya, Harare Zimbabwe, Johannesburg Afrika Kusini
na Lusaka nchini Zambia katika kipindi cha miaka mitatu ya kuendesha shughuli
zake.
“Tangu
tuanze safari zetu tumeshabeba abiria
zaidi ya 1,800,000 ambapo utafiti wetu unaonesha kuwa zaidi ya theluthi moja ya abiria wetu walikuwa ndio mara yao ya kwanza
kumudu kusafiri kwa ndege”, anasema
Corse.
Aliendelea
kusema, “kuongeza ndege nyingine kwenye safari zetu kunatupa fursa muhimu ya kuongeza masafa kwa njia zetu zilizopo ili kukidhi
mahitaji ya wateja, na na inasaidia kwenye lengo letu la kuongeza njia
moja ya kimataifa kwenye mtandao wetu kwa mwaka huu 2016”.
Hali
kadhalika, Corse anabainisha kuwa ndege
hiyo mpya inamanisha kuwa fastjet ni sawia
na ni kubwa katika kutosheleza kupanuka kwa shughuli za fastjet.
Ndege
hiyo A319 ambayo ni Airbus ni ya injini mbili ambazo zinatoa kiwango cha juu cha ufanisi
pamoja na kiwango cha chini kabisa cha madhara kwenye mazingira, ikiwa ni
nyongeza kwenye viwango vya juu vya hali
ya kuliwaza ndani ya ndege hiyo ya kisiasa.
Ndege
hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 156 ambaop wanamudu viwango vya chini vya
kuendesha mtindo wa maisha wa gharama nafuu ambao unaendeshwa na Fastjet
Tanzania.
Baadhi
ya njia muhimu ambazo ndege hiyo mpya
itakuwa inahudumia ni njia mpya
iliyoanzisjhwa hivi karibuni kati ya Dar es Salaam na Nairobi, Kilimanjaro na
Nairobi na Dar es Salaam kwenda Zanzibar
ambazo zote zilianza kwa mara ya kwanza Januari 11, 2016. njia hizi mpya zote ni kielelezo muhimu muda mrefu kwenye
upanuzi wa njia za fastjet kitaifa na
kimataifa.
Fastjet
inatarajia kuongeza ndege zaidi kwenye njia yake ya Kenya kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka
kunakosababisha na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati, na hali
kadhalika imeshajionesha kuwa kuna matarajio ya kuzindua
safari kati ya Zanzibar na Nairobi
na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka 2016.
“Usafiri
wa anga unaoumudu ni muhimu kwenye
kukuza uchumi wa Tanzanoa, hususani kwenye kukuza sekta za biashara na utalii”, alisema
Corse.
Hali
kadhalika Corse alibainisha kuwa ndege
hiyo mpya inamaanisha kwamba ndege za
Fastjet zitatosheleza kiasi cha kutosha
kusaidia kwenye changamoto za usimamizi na uendeshaji iwapo
ndege moja miongoni mwake itakuwa
haifanyi kazi au kama ipo kwenye matengenezo au ukarabati wa lazima.
0 comments:
Post a Comment