Meneja Masoko wa Airtel, Anethy Muga akionyesha moja ya tangazo la
ongezeko la muda wa masaa ya vifurushi vya Airtel yatosha wakati wa kutangaza
muda mpya wa kuisha kwa vifurushi vya Airtel yatosha kwa siku kuwa ni Saa 25.
Yaani Saa 24 ya siku ongeza saa moja.
******************
Airtel Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yake ya kujali wateja wake
kwa kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel Yatosha hivyo kuvifanya kuwa
bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.
Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo, Meneja Masoko wa
Airtel, Aneth Muga alisema "huduma yetu ya Airtel Yatosha
inaendelea kukidhi mahitaji ya Wateja wetu kwani vifurushi tunavyotoa sasa
vya Airtel Yatosha vya siku kwa shilingi 500 tumeongeza muda wake
wa kutumika zaidi ukilinganisha na vifurushi vingine vinavyotolewa
sokoni
Muga alisema sambamba na hili vifurushi vya Airtel Yatosha
vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini wakati wowote Saa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa Saa 24 na 1 la
nyongeza.
Kikubwa na kizuri zaidi bado pia mteja anapojiunga na vifurushi hivi
anapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya promosheni yetu kabambe ya Airtel
Mkwanjika na kujishindia pesa taslimu hadi sh. Milioni moja"
Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa
kupiga *149*99# na kisha kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake. Airtel
yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi.
0 comments:
Post a Comment