Nafasi Ya Matangazo

December 20, 2015

Wafanyakazi wa TBL wa Arusha kutoka vitengo mbalimbali wakiwa wameshikilia kombe la tuzo
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wa Dar kutoka vitengo mbalimbali wakiwa wameshikilia kombe la tuzo
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza wakiwa katika msafara wa kubeba kombe la tuzo kutokea uwanja wa ndege wa Mwanza kuelekea kiwandani lilipowasili mkono humo  mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya    wa TBL wa Mwanza kutoka vitengo mbalimbali wakiwa  wameshikilia kombe la tuzo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wa Mbeya kutoka vitengo mbalimbali wakiwa wameshikilia kombe la tuzo.
**************
Wafanyakazi wa kampuni  ya Tanzania Breweries Limited  Group  katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Arusha wameshiriki kusherehekea mafanikio ya kampuni yao kwa kuibuka  mshindi wa tuzo  ya mwajiri bora kwa mwaka 2015 ambayo ilitunukiwa hivi karibuni na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).

Ushindi huu umekuwa shirikishi kwa wafanyakazi wote ambapo kombe la tuzo hiyo limetembezwa katika viwanda vya kampuni vilivyopo katika mikoa mbalimbali ambapo wafanyakazi walilipokea na kufanya hafla za kusherehekea ushindi huo.

Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa TBL Group David Magese alisema  kuwa ushindi huu na mafanikio mengine ya kampuni hayahusu uongozi pekee bali wafanyakazi wote wa kampuni “ushirikishwaji wa 
wafanyakazi wote katika mafanikio yetu ni jambo ambalo tunalizingatia sana na ndio maana tumeamua kulizungusha kombe hili la tuzo ya mwajiri bora kwao ili washerehekee ushindi huu kwa kuwa ni miongoni mwa wadau wakubwa wa mafanikio haya”.Alisema.

Magese aliongeza kusema kuwa TBL Group ambayo  pia inashikilia tuzo ya Mlipa Kodi bora nchini mbali na ushindi huu wa jumla mwaka huu pia ilishinda tuzo zingine tofauti ambazo ni Uzingatiaji Kanuni Bora
za Uongozi,Uongozi na Utawala,Uzingatiaji wa Kanuni za Raslimali Watu ,Ubora na Uzalishaji,Kujari na kuthamini walemavu na tuzo ya Taasisi Bora inayoongoza kwa Ukubwa.

“Mwaka jana kampuni ya TBL ilishinda tuzo ya jumla katika kipengele cha Mahusiano mazuri na wafanyakazi ambayo inadhihirisha kuwa kampuni imeweka mazingira bora ya kufanyia kazi na inawajali
wafanyakazi wake katika ngazi zote.Tuzo hiyo pia ilitambua kuwa TBL imejenga mazingira bora na uongozi makini unaozingatia vigezo bora vya ajira na kujenga mazingira mazuri ya kazi kwa waajiriwa wake”.

Alimalizia kwa kusema kuwa kampuni hiyo inao wafanyakazi 2,100 nchini kote wakiwa wanafanya kazi za ufundi,Mauzo na Usambazaji,na katika vitengo mbalimbali vya biashara na kati ya hao wapo wenye ajira

za kudumu na ajira za muda na kuongeza kuwa itaendelea kutoa motisha kwa wafanyakazi,kujali afya zao na kuzingatia zaidi kanuni za usalama kazini pia kuwaendeleza wafanyakazi wake kimafunzo ili kuongeza ufanisi zaidi.
Posted by MROKI On Sunday, December 20, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo