Nafasi Ya Matangazo

December 19, 2015

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na watendaqji mbalimbali wa mradi wa mabasi yaendayo haraka waliofika katika kituo cha Feri cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea miundombinu ya DART 
IIMRADI wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) kuanza Januari 10, 2016 hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa wakati akikagua  ujenzi wa miundo mbinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.

Pia Majaliwa amewaagiza watendaji wizara ya Tamisemi ambao ni wamiliki wa mradi huo  kusimamia vyema ili uanze kufanya kazi  kama ilivyo pangwa kwa kuwa mabasi 120 yalishawasili jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ameanza kwa kukagua vituo vya mradi huo kuanzia cha Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na kuwapongeza kwa kumaliza kujenga vituo 15 kati ya 27 na amewaagiza kumalizia vituo vilivyo baki ili kufikia januari 10 mwakani mabasi yaanze kufanya kazi.
Posted by MROKI On Saturday, December 19, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo