Nafasi Ya Matangazo

December 08, 2015

KUNA ule msemo wa watu wa mjini, "Uki-beep, napiga" na kweli leo hii Desemba 8, 2015 pale Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, barabara ya Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, mlipa kodi mmoja alitupia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akiomba wataalamu wa IT wa TRA, wafike haraka kwenye ofisi zao za TRA Barabara ya Samora kwani mitambo ya ku-print Motor Vehicles License ime-collapse", na watu wamekaa tu wasijue la kufanya.
ilichukua kama dakika 15 au 20 hivi, watu wawili waliovalia suti maridhawa na dada mmoja "aliyeshiba", walitinga kwenye ofisi hizo, na kukuta walipa kodi wakiwa wamejazana kwenye mabenchi wakijipepea tu, kutokana na joto kali.
Mmoja wa watu hao waliovalia suti, alianza kuwauliza walipa kodi, "Jamani vipi huduma za hapa mnaridhika nazo."? Aliuliza mmoja wao.
Walipa kodi hao kwanza walimtazama, na mmoja "akajilipua", hapana haturidhiki nazo, hapa unapotuona tumeshakaa sana, huduma hakuna tunaambiwa mtandao haupo, tumeshindwa kuchapishiwa stika za malipo ya kodi ya barabarani.
Mwingine akasema, hata hali ya hewa humu ndani kama unavyoiona joto kali, hakuna viyoyozi, na tumekuja kulipa kodi hii ni sawa??, akahoji mlipa kodi huyo.
Baada ya majibu hayo, Mlipa kodi mmoja aliibuka na kuwaambia wenzake, jamani semeni huyo ndiye bosi mpya wa TRA, "tiririkeni" yaani semeni, na hapo malalamiko yakawa mengi, naye bosi huyo ambaye si mwingine bali ni Dkt. Philip Mpango, ambaye hivi karibuni,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alimteua kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa TRA, akiziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Kamishna Rished Bade, akawajibu, nimeyapokea malalamiko yenu, na ndiyo maana mmeniona niko hapa, nilipokea ujumbe kutoka kwa mlipa kodi akilalamika kuwa hapa kwenye tawi letu huduma zimesimama, nikaona nfike kujua nini kimetokea. Alisema Dkt. Mpango akiwaambia walipa kodi hao ambao walionekana kufurahishwa na maneno hayo.
Wakati akiwaeleza hayo, mitambo hiyo ghafla ikaanza kufanya kazi na waliokuwa jirani na madirisha walianza kuitwa mmoja mmoja na kupatiwa huduma.
Hiyo ndiyo serikali mpya ya awamu ya tano yenye kauli mbiu "Hapa Kazi Tu", hakuna kulala kila mtu anapiga kazi tu.
 "figisu figisu" ya kile wafanyakazi wa hapo waliwaambia wateja wao kuwa "system iko down", yaani kwa maana ambayo wao wamezoea kuwaambia wateja kuwa mtandao wa computer haufanyi kazi kwa hivyo walipa kodi kibao waliokuwepo kwenye ofisi hizo, walilazimika kukaa tu kwenye mabenchi wakimuomba mungu mtandao huo upone ili waweze kupata "stika" za magari yaani Motor Vehicles License .
Pichani Dkt. Mpango (kushoto), akizungumza na walipa kodi hao kwenye tawi la TRA, barabara ya Samora Desemba 8, 2015
Posted by MROKI On Tuesday, December 08, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo