Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania (TASO), Engelbert Moyo akizungumza katika moja ya mikutano yake. Kushoto ni Katibu Mkuu Imani Kajula. picha ya Maktaba.
**********
Moja ya vyama muhimu katika
kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini Tanzania ni Tanzania Agricultural
Organisation (TASO). Pamoja na majukumu mengine, TASO ndio wamiliki na
wasimamiaji wamaonyesho ya nanenane Nchini Tanzania. Hadi sasa TASO ina viwanja
vitano vya maonyesho ya nanenane kwenye kanda za Kaskazini-Arusha, kandayalati
–Dodoma, Mashariki – Morogoro, NyandazaJuu –Mbeya na Kanda ya Kusini – Lindi.
Mfumo wa utendaji wa TASO umeanzia kwenye Kata, Wilaya, Mkoa, Kanda
naTaifa.
Juhudi zinafanyika kuanzisha
viwanja vya maonyesho kwenye kanda ya Magharibi na kanda ya ziwa katika muda
mfupi ujao. Tanzania ikiwa inatumia si zaidi ya asilia 25% ya Aridhi inayofaa
kulimwa, Kilimo kinabakia kuwa msingi muhimu wa kukuza uchumi na ajira Nchini
Tanzania. Pia izingatiwe kuwa Tanzania ina jumla asilimia 46% ya aridhi yote ya
Afrika Mashariki hivyo kuwa na fursa kubwa ya kukuza soko na kulisha nchin
yingine za Afrika Mashariki na nje.
Jumamosi yaTarehe 14 Novemba 2015
mjini Dodoma, TASO ilifanya uchaguzi wa viongozi wa Taifa ambao wataongoza
taasisi hii muhimu katika kukuza kilimo kwa miaka 5. Viongozi waliochaguliwa ni
Engelbert Moyo – Mwenyekiti, SharifaAbebe – Makamu Mwenyekiti, Imani Kajula –
Katibu Mkuu, Daudi Mwalusyamba – Katibu Mkuu Msaidizi na Michael Lupyana –
Mweka Hazina.
Akizungumza baada ya kuchaguliw
aMwenyekiti wa TASO Taifa Engelbert Moyo alisema ‘’ Huu ni mwanzo mpya wenye
malengo ya kuchochea mchango wa kilimo katika Uchumi, Maisha ya Watanzania,
weredi katika kilimo na ajira. Ni fursa adhimu kuwa na viongozi waTaifa wenye
ujuzi katika fani mbalimbali; Kilimo, Biashara, Masoko naFedha. Naamini kuwa
TASO itapiga hatua kubwa katika kuwa muda muhimu katika kutoa mchango katika
sekta hii nyeti’’.
Nae Katibu Mkuu wa TASO Imani
Kajula alisema ‘’ Kilimo ni sekta yenye kuajiri watanzania wengi, lakini
imekuwa na changamoto nyingi, tunatambua kazi hii tuliyopewa ni adhimu na
muhimu katika kuleta mabadiliko ya kukuza soko la mazao, ubunifu watechnojia
rahisi za kilimo, upatikanaji wa habariza kilimo, uvuvi, ufugaji na masoko kwa
wakulima na pia kuboresha maonyesho ya Nanenane kuwa jukwaa la kuchochea ukuaji
wa kilimo na ajira’’.
0 comments:
Post a Comment