Mwanamitindo wa hapa nchini, Mustafa Assanali kulia na Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, Godfrey Mngereza wakifungua pazia kuzindua Onesho la Swahili Fashion Week leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam aambalo litakuwa na mwendelezo wa kuonesha ubunifu wa mitindo kwa siku tatu mfululizo litakalokuwa likifanyika katika hoteli ya Sea Clief jijini Dar es Salaam.
IKIWA tunakaribia mwisho wa
mwaka 2015, onyesho rasmi la mavazi Swahili Fashion Week linakuletea pande za
siku tatu za mitindo, urembo, na mitindo ya maisha katika eneo moja la tukio
kukiwa na onesho lisilosahaulika na kuwa na tamaduni mbalimbali ambazo
zinaendelea kuifanya Tanzania kuzidi kuangaliwa kimataifa. Hivyo kila wiki ya
kwanza ya mwezi wa desemba barabara zote zinaongoza kuelekea jiji la Dar es
Salaam, tangu sasa katika uzinduzi wa Swahili Fashion Week 2015, huu utakuwa
mwaka wa nane wa maonesho haya.
Mwanzilishi wa onyesho hili la
mavazi Swahili Fashion Week alisema Mustafa Hassanali alisema “kuna methali inasema ” “kama unataka kwenda haraka nenda
mwenyewe, kama unataka kwenda mbali nenda pamoja” mwaka huu tuna nia ya kufikia
jamii kusisitiza na kukuza vipaji katika
tasnia ya mitindo na zinginezo. Tuna nia ya kukuza thamani ya bidhaa, kupigania
dhana ya bidhaa zinazotangenezwa afrika na kujenga bidhaa zenye mizizi ya
afrika.
Msimu wa nane wa onesho la Swahili
Fashion Week utaendelea kuwa mwangaza wa maonesho ya week ya mavazi kote
Afrika,ndani ya Tanzania pamoja na nchi za nje ,huku wabunifu wakipatiwa hisia
kutoka kwa vyombo vya habari vya kitaaifa na kimataifa toka onesho hili
lilipoanzishwa mwaka 2008.Swahili Fashion Week limekuwa jukwaa kuu la ubunifu
kwa wabunifu kuanziaAfrika ya Mashariki na kati ambao wameonesha kazi zao kote
ulimwenguni kwa kila hadhira.
“tunaendelea kuwaomba jamii kukuza
Tasnia ya ubunifu na kuvaa fahari ya
vilivyo tengenezwa za Afrika hasa dhana
ya Kitanzania. Vipaji vya ndani vinahitaji kulelewa na kuvihusisha bidhaa zinazotambulika ulimwenguni, kutoa ni
moyo si utajiri, hivyo tunatazama mbele katika kuanza kuwasaidia kampuni ndogo ndogo na mashirika
hili kuwezesha biashara hii ya mitindo ya ubunifu.” Alisema msimamizi wa
Swahili Fashion Week ,Honest Nyamai.
Onesho la Swahili Fashion Week
litafanyika kuanzia tarehe 4 mpaka tarehe 6 desemba katika hotel ya Sea cliff
wabunifu 24 watapata nafasi ya kuonyesha nguo zao kila jioni ya siku zote 3 za
onesho kuanzia saa 2:30 usiku na kuendelea. Katika kipindi cha mchana cha siku
zote tatu kutakuwa na maonesho ya bidhaa, ambapo washiriki mbalimbali
wataonesha na kuuza kazi zao zilizotengenezwa na mkono, za sanaa, na vidani.
Siku ya mwisho itaishia na sharehe za kutangazwa kutoa tuzo kwa washindi wa Tasnia ya mitindo
katika Nyanja 21 tofauti.
Swahili Fashion Week 2015 na
Tuzo limeandaliwa na 361 degrees, kushereheswa na sea cliff hotel na
kudhaminiwa na EATV, East Africa Radio,
Jaguar “The Art of Performance”, CMC, Vodacom Tanzania, Tanzania Printers Ltd,
A1outdoor, 2M Media, BASATA (Baraza La Sanaa La Taifa), NexiaSJ, Green Telecom,
Fabcars, Asila Make up, Raha, Eventlites na Darling Tanzania
0 comments:
Post a Comment